Friday, March 7, 2025

Benki ya NBC Yaandaa Hafla ya Futari Zanzibar, Yajivunia Ongezeko la Wateja
Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar, Zubeir Ali Maulid (katikati) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw Rayson Foya (kushoto) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar jana. Kulia ni Meneja wa Benki ya NBC tawi la Mbeya Bw Bw Abdul Karim Mkila.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa hafla ya futari mahususi kwa wateja wake wa Kiislamu Zanzibar huku ikijivunia ongezeko la wateja kwa zaidi ya asilimia hamsini mwaka huu kutoka idadi ya m waka uliopita.
Hafla hiyo imefanyika jana Hotel Verde, Zanzibar ikiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar, Zubeir Ali Maulid. Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw Rayson Foya alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi kwenye hafla hiyo iliyohudhiriwa na wateja, viongozi wa serikali pamoja wafanyakazi wa benki ya NBC.
Katiba hotuba yake Spika Zubeir aliipongeza benki hiyo kwa muendelezo wake wa kutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kujenga mahusiano yake na wateja wenye imani ya Kiislam, hatua aliyoitaja kuwa imekuwa ngunzo muhimu katika ustawi wa biashara sambamba na kuchochea uchumi jumuishi kupitia huduma bora za kibenki.
“Ni wazi kwamba benki ya NBC wanatambua kuwa Ramadhan ni nguzo muhimu ya imani ya Kiislamu, wakati wa ibada, upendo, na sadaka. Hivyo kwa kutambua thamani hiyo, futari hii ni ishara ya kuthamini mahusiano yao na sisi wateja wao na wadau wao, ikiwa ni njia mojawapo ya kushirikiana pamoja baraka za mwezi huu.’’ Alisema Spika Zubeir
Akizungumzia mafanikio na ongezeko la wateja hao, Bw Foya alisema limechochewa zaidi na mahusiano mazuri baina ya benki hiyo na wateja visiwani Zanzibar hususani kupitia utoaji wa huduma unaozingatia misingi ya Sharia za La’ Riba sambambamba na maboresho ya huduma za benki hiyo hususuani kwa njia kidigitali.
“Katika kuthibitisha dhamira yetu kwenye maboresho ya huduma zetu ni hivi karibuni tu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizindua rasmi ‘App yetu ya NBC Kiganjani ikiwa na maboresho makubwa zaidi kulingana na mahitaji ya wateja wetu ambao sasa wanaweza kufungua akaunti popote walipo, kufanya malipo ya serikali (GEPG), kununua umeme (LUKU), na kulipa ankara mbalimbali kwa urahisi. Nawaalika wote kupakua NBC Kiganjani App kutoka Google Play Store au Apple App Store na kufurahia huduma hii ya kisasa.’’ Alisema.
Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa zawadi kwa wageni waalikwa huku pia ikitoa wasaa kwao kubadilishana mawazo na kufurahia pamoja wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (katikati) akishiriki Dua ya shukrani wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw Rayson Foya (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Baadhi ya waageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC Zanzibar wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wateja wa benki ya NBC visiwani Zanzibar wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
JUBILEE HEALTH INSURANCE YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE,YAPEWA TUZO YA TSEA 2025
Hassani MakeroApr 08, 2025ABSA YAZINDUA MKOPO MPYA WA MALI ZA KIBIASHARA,SERIKALI YAPONGEZA JITIHADA
Hassani MakeroApr 04, 2025AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAPELEKA TABASABU KITUO CHA KULELEA WATOTO CHAKUWAMA
kilole mzeeMar 28, 2025
Labels:
BIASHARA
Location:
Zanzibar, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment