AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAPELEKA TABASABU KITUO CHA KULELEA WATOTO CHAKUWAMA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Friday, March 28, 2025

demo-image

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAPELEKA TABASABU KITUO CHA KULELEA WATOTO CHAKUWAMA

.com/img/a/
Akiba Commercial Bank Plc Yapeleka Tabasamu Kituo cha Kulea Watoto- Chakuwama Sinza Dar es Salaam, 28/03/2025 – Katika kuendelea kujitoa kwa jamii, Akiba Commercial Bank Plc imetoa msaada kituo cha kulea Watoto cha Chakuwama, ikilenga kuboresha ustawi wa watoto na kuleta tabasamu kwenye nyuso zao.

Msaada huu, ambao unajumuisha mahitaji muhimu, unaonesha dhamira ya Benki hiyo ya kusaidia wenye uhitaji na kujenga matumaini kwa mustakabali mwema.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Bi. Dora Saria, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Bank, alieleza kuwa Benki hiyo inaamini katika kuunga mkono jamii na kuleta mabadiliko chanya ya kudumu.

"Akiba Commercial Bank, tunaamini katika nguvu ya mshikamano katika kubadili maisha. Msaada huu ni hatua muhimu ya kuhakikisha ustawi wa watoto hawa na kuleta matumaini kwa wenye uhitaji kwa maisha bora yajayo," alisema Bi. Saria.
.com/img/a/
Kwa upande wake, Bw. Hassan Tabu, mwakilishi wa Kituo cha Chakuwama, aliishukuru Akiba Commercial Bank kwa ukarimu wake, akibainisha kuwa msaada huo utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watoto hao.

"Tunaishukuru sana Akiba Commercial Bank kwa kusimama nasi. Msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watoto na kuwapatia sababu ya kutabasamu," alisema.
.com/img/a/
Kupitia juhudi hizi, Akiba Commercial Bank Plc inathibitisha tena dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii kwa vitendo, ikilenga kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu kwa jamii inayoihudumia.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *