Thursday, January 11, 2018

SERENGETI LITE MDHAMINI RASMI LIGI YA SOKA LA WANAWAKE
Mkurugenzi Mtendaji wa
SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakisaini mkataba
wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite
ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Ofisa mkuu wa michezo wa wizara
ya habari, utamaduni,sanaa na michezo Henry Lihaya (katikati waliosimama)
akishuhudia tukio la kusaini Mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya Wanawake
kupitia kampuni ya Serengeti Breweries Ltd.Mkataba huo umesainiwa kati ya SBL
(Mkurugenzi Mtendaji wake ni Helene Weesie) na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania TFF (,Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura).Ambapo SBL itatoa jumla
ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450) ili kuzidhamini timu zote
zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu .
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene
Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakipongezana mara baada ya
kusaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti
Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Dar es
Salaam, Januari 10 2018: Bia pendwa ya Serengeti Premium Lite, ambayo
inazalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), leo imetangaza kuwa mdhamini
rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake (Women Premier League). Katika
Mkataba uliosainiwa kati ya SBL na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili
kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka
mitatu ijayo.
Kama mdhamini rasmi wa ligi hiyo, Serengeti Premium Lite itatoa
msukumo kwa timu zote nane za wanawake kwenye ligi ambapo mshindi atakuwa
mwakilishi wa taifa katika mashindano ya kikanda na ya kimataifa. Kupitia
udhamini huo, SBL ina matumaini makubwa kwamba itaweza kuwazindua wananchi na
hasa mashabiki wa soka na kuwaunganisha pamoja ili kuongeza hamasa katika ligi
ya taifa ya wanawake kupitia bia hiyo kipenzi cha watanzania ya Serengeti
Premium Lite.
“Tunayo furaha kubwa kuwa
wadhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake kupitia bia yetu maarufu
ya Serengeti Lite. Siku zote tumekuwa tukiamini katika kuendeleza vipaji katika
sehemu mbali mbali za nchi na haswa inapokuja katika michezo inayotuleta
pamoja. Tunaamini udhamini wetu utawavutia mashabiki wa rika mbali mbali
kuiunga mkono ligi ya wanawake na kufikia mafanikio makubwa,” alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, SBL inaamini katika nguvu ya mpiga
wa miguu ambayo inawaunganisha watu.
Udhamini wa Twiga Stars unafuatia historia ndefu ya udhamini wa
timu ya soko ya wanaume, Taifa Stars ambayo mpaka hivi sasa inaendelea kupata
udhamini wa SBL kupitia bia yake mama ya Serengeti Premium Lager. SBL ni sehemu
ya kampuni ya Diageo ambayo inauhusiano mkubwa na masuala ya soka duniani ikiwa
ni pamoja na udhamini wa Ligi Kuu ya Uingereza kupitia bia ya Guinness.
Kwa upande wake Makamu wa
Rais wa TFF Michael Wambura alisema; “Leo kwa mara nyingine tunashuhudia
ushikiano muhimu kati yetu na SBL, kampuni maarufu ya bia na ambayo imekuwa
mstari wa mbele kwa kusaidia maendeleo ya michezo nchini. Ushirikiano huu
utasaidia sana katika kuendeleza soka letu la wanawake pamoja na mashindano
tutakayokuwa tunaandaa. Tunafurahia udhamini huu kupitia bia ya Serengeti Lite
na tunaamini utakuwa wa mafanikio makubwa,”
Utiaji saini kati ya pande hizo
mbili ulishuhudiwa na Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni
na Michezo, Bw, Yusuph Singo ambaye aliipongeza SBL kwa kujitolea kwake katika
kuunga mkono sekta ya michezo nchini na pia kuwataka Watanzania wenye mapenzi
mema pamoja na makampuni mengine kuiga mfano mzuri wa kampuni ya SBL.
Tags
# MICHEZO
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Benki ya Mwalimu Commercial Plc yazindua akaunti ya Tukutane Januari, kuboresha maisha ya watanzania.
Older Article
JIJI LA DAR LASHINDA TUZO YA KWANZA BARANI AFRIKA YA HUDUMA BORA YA USAFIRI ENDELEVU MWAKA 2018 JIJINI WASHINGTON, D.C., MAREKANI
TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
Hassani MakeroMar 08, 2025WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA KUSHIRIKI MBIO ZA YAS KILI INTANATION HALF MARATHON
kilole mzeeFeb 15, 2025KOCHA WA YANGA APEWA MKONO WA KWAHERI
Hassani MakeroFeb 04, 2025
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment