Katika muendelezo wa ubunifu wa matumizi ya teknolojia ambayo yanarahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa urahisi, Benki ya Standard Chartered Tanzania imezindua mfumo mpya wa matumizi ya teknolojia ya kidigititali ambayo inawezesha wateja wake kupata huduma zaidi ya 70 za kujihudumia wenyewe pamoja na huduma mbalimbali za kibenki kwa urahisi.
Mfumo huu unawezesha wateja wa Benki ya Standard Chartered kujipatia huduma za kibenki kulingana na matakwa yao. Kupitia huduma hii, mtu yeyote anaweza kujiunga na Benki ya Standard Charted kwa kuanza na kupakua programu hii.
Kupitia huduma hii, wateja wanaweza kufurahia ofa mbalimbali kama vile kutotozwa malipo katika kulipa ankra ,malipo ya akaunti ya mwezi, kutokuwepo kwa kiwango cha akiba ya kufungua akaunti, matumizi ya mashine za kutoa fedha (ATM) au kadi za kutolea fedha na mihamala ya kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao kwenye akaunti za Standard Charted.
Mfumo huu wa kidigitali wa Standard Chartered umelenga kuwapatia wateja fursa ya kufurahia huduma za kibenki zaidi kupitia njia za kisasa zinazorahisiha maisha, mtu yeyote anaweza kujiunga na Benki kwa kupakua Programu hii kupitia simu yake ya mkononi .
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani alisema, “kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa huduma bora kwa wateja wetu. Tunayo furaha kuzindua programu hii ya kurahisisha zaidi upatikanaji wa huduma za kibenki hapa nchini Tanzania. Huu ni mwendelezo wa safari yetu muhimu ya matumizi ya teknolojia za kidigitali kama Benki na kudhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kuwekeza katika kuleta mapinduzi ya kiteknolojia za kisasa, kujenga mifumo na kuimarisha watu wetu tukiendelea kutumia mifumo yetu na ujuzi wa ngazi ya kimataifa kuleta mabadiliko ya uhakika ya matumizi ya teknolojia ya kidigitali nchini Tanzania.
Aliongeza kusema, “Matumizi ya teknolojia za kisasa za kidigitali kwetu kuna maana ya kuleta mapinduzi kutoka mifumo ya utoaji wa huduma za kibenki ya zamani kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja. Tunahakikisha tunabadilika kwendana na matakwa ya wateja sambamba na mabadiliko yaliyopo kwa wakati huu,’’.
Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za kibenki wa Standard Chartered, Ajmair Riaz alisema, wateja wa zama za sasa wanahitaji kupata huduma bora na wanatafuta huduma na washirika ambao wanaweza kuwapatia huduma zinazopatikana kirahisi, kwa gharama nafuu .
"Programu hii yetu mpya imebuniwa kuleta suluhisho kwa matakwa haya yote ya wateja baada ya kufanyia kazi maoni yao kuhusu nini wanahitaji, itawawezesha kupata huduma zote za kibenki kupitia simu zao za mkononi kwa urahisi, kwa mara ya kwanza katika safari yetu hii ya kuleta mapinduzi ya teknolojia ya kidigitali katika upatikanaji wa huduma za kibenki, mteja anaweza kufungua akaunti ndani ya muda wa dakika 15 kupitia mfumo huu,” aliongeza.
Benki ya Standard Chartered inafanya kazi na msanii maarufu wa Tanzania, Vanessa Mdee ambaye atakuwa ni balozi wa huduma hii kwenye promosheni mbalimbali.
Programu inaweza kupakuliwa au kuboreshwa kupitia Progamu za simu za kisaa za Google play store au Apple Store na baada ya zoezi hilo mtu anaweza kufungua akaunti ya Benki ya standard Chartered kwa njia ya mtandao ndani ya muda usiozidi dakika 15.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dk. Bernard Kibesse,akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa programu ya Standard Chartered Tanzania Digital App.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya uzi nduzi wa programu ya Standard Chartered Tanzania Digital App uliofanyika katika hoteli ya Hyatt.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Kibesse (Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani,Balozi wa Programu mpya ilizozinduliwa,Vanessa Mdee na Mkuu wa huduma za kibenki wa wateja wadogo wa Benki hiyo, Ajmair Riaz ,wakionyesha miondoko ya UNSTOPABLE wakati wa hafla ya uzinduzi
No comments:
Post a Comment