Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual yasaidia watoto wenye mahitaji maalum - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, March 11, 2019

Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual yasaidia watoto wenye mahitaji maalum


Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Tanzania
Jabir Kigoda ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya mifuko 400 ya shule kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk. Ave Maria Semakafu ( wa nne kushoto) , iliyotolewa na UAP kusaidia  watoto wenye mahitaji  maalumu katika hafla iliyofanyika Muheza, Tanga, hivi karibuni. Anayeonekana nyuma ya Naibu Katibu Mkuu  ( mwenye hijab) ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza  Mwanasha Tumbo.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo akiongea katika hafla hiyo ya makabdhiano.Kulia kwake ni Meneja wa Uendelezaji Biashara na Masoko wa UAP Jabir Kigoda, na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Ave Maria Semakafu.
 Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Tanzania , Jabir Kigoda ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya mifuko 400 ya shule kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk. Ave Maria Semakafu ( wa tatu  kushoto) , iliyotolewa na UAP kusaidia  watoto wenye mahitaji  maalumu katika hafla iliyofanyika Muheza, Tanga, hivi karibuni. Anayeonekana nyuma ya Naibu Katibu Mkuu  ( mwenye hijab) ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza  Mwanasha Tumbo
Watoto wenye mahitaji maalum wakiwa  kwenye picha ya pamoja  na naibu katibu mkuu, mkuu wa wilaya na viongozi wa UAP baada ya kupokea msaada.

Watoto walio na mahitaji maalum Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga hivi majuzi walipatiwa msaada wa mifuko  400 ya shule na kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Insurance  Tanzania, ikiwa ni kutimiza azma ya kampuni hiyo ya kutoa misaada kwa kundi hilo la watoto.

Msaada huo, wenye lengo la kunyanyua ushiriki wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum, ulitolewa na Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa UAP katika hafla iliyofanyika Muheza,  huku ukipokelewa kwa niaba ya walengwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Ave Maria Semakafu .

“ Sisi katika kampuni ya UAP tunaamini kuwa elimu siyo tu ni  nguzo ya mafanilkio ya binadamu, bali pia ni haki ya msingi ya mtoto, wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum kama hawa, ”alisema Kigoda wakati wa kukabidhiana msaada huo.

Vilevile Kigoda alichukua fursa hiyo kuwaasa wadau katika sekta mbalimbali nchini kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa misaada kama hiyo,  kwa kuwa siyo tu itawawezesha watoto bali itachagiza harakati za utekelezaji wa sera ya taifa ya elimu bure.



Kampuni ya UAP, yenye matawi maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Kahama, Zanzibar, Morogoro and Mtwara,ni moja kati ya makampuni ambayo yameweka kipaumbele katika kuwekeza kwenye misaada ya kuchangia maendeleo ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages