

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepokea hundi ya shilingi millioni 200 kutoka kwa Balozi kutoka katika nchi za falme za Kiarabu balozi Khalifa Abdulrahman Al-Marzooqi leo jijini Dar es Salaam ili kutimiza ahadi yake ya kusomesha watoto wakike 100 waliomaliza kidato cha nne na kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
Rc Makonda amesema jambo alilolifanya sio jambo linalohusiana na siasa bali ni jambo linalosimamia maendeleo katika Mkoa huo, ili kuhakikisha watoto wakike wanapata nafasi ya kupata elimu, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais Dkt.John Pombe Magufuli
“Balozi amejitolea kulipa ada za watoto 100 pamoja na sare za Shule kwa watoto wakike waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi, na nimeanza na hawa mwakani pia zoezi hili litakuwa ni endelevu lento ni kuhakikisha tunaunga mkono jitihadi za Rais wetu katika kukuza elimu yetu,hili jambo sio la kisiasa ni jambo la kusaidia watoto ili kuleta Maendeleo ya nchi yetu” amesema RC Makonda.
Amesema amemuomba Balozi Al-Marzooqi kujenga uwanja wa mpira wa Kikapu utakaoweza kuingiza idadi ya Watu 1000 Mpaka 2000 ambapo amesema amekubali zombi hilo ambapo mpaka sasa yupo katika mikakati ya kuwasilisha ramani kwa Balozi ili kuweza kupata uwanja utakao toa nafasi kwa wachezaji wa kikapu.
Naye Balozi wa Al-Marzooqi amesema wapo tayari kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Elimu, na Afya, amesema ana imani ifikapo mwakani Rc Makonda ataendelea kufanya mambo ya Maendeleo zaidi katika nchi yake.
“Nimpongeze Mkuu wa Mkoa kwa maendeleo anayoendelea kuyafanya katika muungano mzuri wa nchi hizi mbili tutaendelea kusapoti maendeleo ya elimu pamoja na jamii, ninategemea mwakani ataweza kufanya mambo mengine makubwa” amesema Al-Marzooqi .
No comments:
Post a Comment