Spika wa
Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa pale ugeni kutoka benki hiyo
ulipomtembelea ofisini kwake Bungeni
Jijini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Prof. Lucian
Msambichaka.
Spika wa
Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya
Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (katikati) pale ugeni kutoka benki
hiyo ulipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Ndg. Godfrey Ndalahwa
Spika wa
Bunge, Mhe. Job Ndugai (Katikati), akizungumza na ujumbe kutoka benki ya DCB
ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Prof. Lucian Msambichaka (kushoto kwake) ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma
jana.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto),
akisalimiana na Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Dodoma, Joseph Njile wakati yeye
na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni,
Dodoma jana. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian
Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara,
James Ngaluko.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto),
akisalimiana na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James
Ngaluko wakati yeye Mwenyekiti wa Bodi,
Prof. Lucian Msambichaka na Mkurugenzi
Mtendaji, Godfrey Ndalahwa (kulia kwake), wakimtembelea mheshimiwa Spika,
osifini kwake Dodoma jana.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na ofisa Uhusiano wa Benki ya
Biashara ya DCB, Nuru Ashraf, wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo
ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma juzi. Kutoka wa pili kushoto
ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey
Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto),
akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha
Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, wakati
yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake,
bungeni, Dodoma juzi. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof.
Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa
Biashara, James Ngaluko.
Spika wa
Bunge, Mhe. Job Ndugai (Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka
Benki ya Biashara ya DCB ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Prof.
Lucian Msambichaka (wa tatu kulia) walipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni
Jijini Dodoma jana.
Benki ya
Biashara ya DCB imetoa shukurani kwa waheshimiwa wabunge pamoja na mheshimiwa
spika kwa kufanikisha zoezi la uuzwaji wa hisa zao lililofanyika hivi karibuni
kwa mafanikio.
Akizungumza wakati wa mahojiano maalumu jijini
Dodoma leo sambamba na ziara ya uongozi wa juu wa DCB ulioongozwa na Mwenyekiti
wao wa Bodi bungeni juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema
wabunge kama wawakilishi wa wananchi wamesaidia sana kwa taarifa za uuzaji wa
hisa zao kuwafikia wananchi wengi.
Alisema mafanikio ya uuzaji wa hisa
yaliyoifanya benki kuongeza mtaji wake yatasaidia mpango mkakati wao wa kutanua
wigo wa huduma zao wakitarajia ndani ya miaka mitano kuwafikia watanzania wengi
huku wakiwekeza zaidi katika huduma za kidigitali.
“DCB ilianza mpango wake wa kujitanua kutoka
jijini Dar es Salaam miaka miwili iliyopita, safari ya kujitanua inaendelea,
tumeshafika Dodoma na maeneo ya karibu, mfumo wetu unaotusaidia ni kutoa huduma
bora kwa bei nafuu tukiwekeza zaidi katika mfumo wa kidigatali hivyo kuwa na
matawi machache na kuweka vituo vingi vya huduma sehemu mbalimbali nchini,”
alisema.
Zoezi la uuzwaji wa hisa za dcb lilizinduliwa
Novemba 12,2018 na kuhitimishwa Januari 31, 2019 ambapo hisa 36,635,435
ziliuzwa ikivuka kiwango cha hisa 33,913,948 zilizopangwa awali.
Dcb is coming up very aggressively in the banking industry
ReplyDeleteBig up