Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto james na maofisa wa Wizara alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie akiongea na wanahabari akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na maofisa wa Wizara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
Baada
ya mazungumzo hayo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
amewahakikishia Watanzania kuwa wizara yake imejipanga kutoa ufafanuzi wa
maeneo yote ambayo yanapaswa kuwemo katika taarifa yaIMF ya ukuaji wa uchumi wa
Tanzania ikiwemo utelezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi.
“Ili
uchumi wa nchi ukue ni lazima uwe unawekeza, na bahati nzuri sana Mhe. Rais
amemueleza mgeni wake jinsi tunavyowekeza kwenye miundombinu hususani ujenzi wa
reli ya kati, jinsi tunavyowekeza katika ujenzi wa bwawa kubwa litakalotupatia
megawati 2,100 za umeme na pia miradi ya barabara na viwanda vingi
vilivyojengwa, haya ndio yanayokuza uchumi na sisi tunaamini kabisa wenzetu
hawakuyazingatia kabisa katika taarifa ya awali (iliyovuja)” amesema Dkt.
Mpango.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi
amewatoa shaka wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuendelea kuwa na imani na
mazingira ya uwekezaji ya Tanzania na amewataka Watanzania kutokua na hofu
kwamba wawekezaji watapungua kwani wawekezaji hao wanaendelea kuja.
“Nashukuru kwamba hata wawekezaji wenyewe hawana hofu
kwani hata baada ya taarifa hiyo kuwa imevujishwa bado wengi wameendelea kuja
na kuonesha nia ya kufanya kazi na sisi, na nashukuru Shirika la Fedha la
Kimataifa kwa kuja kuzungumza na sisi, hiyo ni dalili kuwa shirika hili bado
lipo nasi na bado tunaendelea na mazungumzo" Amesema Prof Kabud na
kuongeza kuwa "Wale ambao walidhani pana ugomvi mkubwa kati ya Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF) na Tanzania walikuwa wamekosea kabisa,na msimamo wa
Tanzania utafahamika baada ya mazungumzo kuanza na kuweza kuwapitisha katika
miradi mikubwa ya maendeleo ambayo inafanyika” amesema Prof. Kabudi.
Kwa upande wake Selassie amesema aliomba
kukutana na Rais Magufuli ili kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu
uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na IMF na jinsi shirika hilo
linavyoshiriki katika kutoa ushauri wa kiuchumi.
Selassie
amempongeza Rais Magufuli na Serikali anayoiongoza kwa juhudi kubwa
zinazofanywa kuwekeza katika miradi mikubwa ikiwemo miundombinu itakayopunguza
gharama za nishati ya umeme.
Kuhusu
kuvuja kwa taarifa za ukuaji wa uchumi, Selassie amesema IMF itatuma timu ya
wataalamu wake itakayokutana na timu ya wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango
ya Tanzania kwa lengo la kupitia maeneo yote yaliyoanishwa katika matazamio ya
ukuaji uchumi ya IMF na yale ya Serikali ya Tanzania.
“Mimi
na Rais Magufuli tumekubaliana kuwa IMF na Tanzania watabaki kuwa wadau
wanaoaminiana, tunaona fursa nyingi na muhimu katika nchi hii ikiwemo mipango
mizuri ambayo Rais Magufuli ameianzisha.” Amesema Selassie na kuongeza kuwa
“Katika
wiki zijazo, tutaendelea na mazungumzo na kuendeleakufanya kazi kwa ukaribu na Serikali
ya Tanzania na tutaleta timu ya wataalamu watakaokuja kujadiliana na Serikali
ya Tanzania ili kutazama maeneo yote yaliyofanyiwa mageuzi makubwa na
kuyawianisha na ukuaji wa uchumi” amesema Selassie.
No comments:
Post a Comment