MBUNGE KABATI AWAWEZESHA WANAFUNZI WA UKWATA LUNGEMBA KUREKODI ALBAMU YAO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Sunday, July 7, 2019

demo-image

MBUNGE KABATI AWAWEZESHA WANAFUNZI WA UKWATA LUNGEMBA KUREKODI ALBAMU YAO

2-22-1024x683
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Rita Kabati ametoa msaada kwa mmoja ya wanafunzi wa chuo cha Rungemba walipofanya mahafari ya kidini. (Picha na Mpiga Picha wetu) 
1-30-1024x683
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa(CCM) Rita Kabati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii Rugby (hawapo pichani) wakati wa mahafali ya ukwata. (Picha na Mpiga Picha wetu) 


MBUNGE viti maalum mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati amechangia shilingi laki mbili (2) na kuahidi kununua kifaa cha muziki kwa wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya jamii, Lungemba, Mufindi zitakazotumika katika kurekodia albamu yao.

“Nitachangia shilingi laki 2 kwanza ili mmalize kurekodi nyimbo zenu za video. Na pia nitachangia kifaa cha muziki nitajaribu kutafuta cha aina gani kisha niwaletee”

Mhe. Kabati amechangia fedha hio wakati wa mahafali ya wanafunzi wa dhehebu la Ukwata, chuoni hapo.Pamoja na mchango huo, Kabati amewataka wanafunzi wa chuoni hapo kujikita katika mambo ya kimaendeleo ikiwepo mafunzo ya ujasiriamali yatakayoweza kunyanyua kipato chao.

“Msiache kujiingiza katika mafunzo ya ujasiriamali mtakaposikia yanafanyika kwa sababu yatainua kipato chenu”

Awali akisoma risala kwa mgeni mwanafunzi anayehitimu, Grace Mhanga amebainisha changamoto zinazowakabili wanaukwata chuoni hapo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya muziki, laptop pamoja na pesa taslimu shilingi laki 2 kwa ajili ya kurekodia video.

“Sisi kama wanaukwata tunakosa pesa shilingi laki mbili pamoja na vifaa vya muziki vitakavyosaidia kuendeleza injili ya MUNGU”

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *