Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyaya (kulia), akisalimiana na
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, wakati wa Maonesho ya
Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa
wadhamini. Maonyesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Majimaji mjini Songea
mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akisaini kwenze
kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda
na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini.
Maonesho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Majimaji mjini Songea MKoani
Ruvuma mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto kwa waziri ni Meneja wa Benki
ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, Ofisa Mauzo, Jennifer Peter, pamoja na
Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Hilaria Mhagama alipotembelea banda la
Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma
ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto ni Meneja
wa Benki ya NBC Tawi la Songea Simon Ntwale, na Ofisa Mauzo wa benki hiyo,
Jennifer Peter.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana
mikono na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Jennifer
Peter alipotembelea banda la NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na
Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili
kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale pamoja na
Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC Songea, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwezeshaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema Maonesho ya Viwanda na
kongamano la uwekezaji Ruvuma litaleta fursa nyingi za kibiashara na uchumi
mkoani humo imeelezwa mjini Songea mwishoni mwa wiki.
Alisema Mkoa wa Ruvuma umejaliwa
kuwa na fursa nyingi sana na kwa muda mrefu hawakuwa wakifanya tukio kama hilo
lakini sasa kupitia kongamano hilo litawafungua kuwafahamisha watu
mbalimbali kuwa nini kinapatikana mkoa huo wa Ruvuma.
Alisema changamoto zinazowakabili
wawekezaji wadogo ni pamoja na upatikanaji wa mitaji lakini kwa sasa mkoa
wa Ruvuma umepata mkombozi hususani Benki ya NBC ambayo inatoa mikopo mikubwa
na midogo kwa masharti nafuu sana kinachotakiwa ni uaminifu.
"Nawakaribisha sana
wawekezaji na wadau wote ambao wana nia thabiti ya kuja kuwekeza Ruvuma
kwani mkoa huu umekuwa na nishati ya umeme ya kuridhisha inayoweza kukidhi
mahitaji," alisema.
Kwa upande wake Meneja wa Tawi la
NBC Songea,Simon Ntwale amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa fursa nzuri kwa
Benki ya NBC kwa sababu wameweza kukutana na wadau mbalimbali watakaoweza
kufungua fursa mbalimbali za kibiashara.aziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa huo amesema
kuwa Ruvuma itakuwa na wawekezaji mbalimbali.
Alisema NBC imepata faida ya
kuingia mkataba na taasisi ya PASS ambapo wanakwenda kuwawezesha wakulima
kupata mikopo ya kilimo ambapo mkopaji anaweza kupata pembejeo za kilimo.
Ntwale pia amewatoa shaka wakulima
wakubwa na wadogo pamoja na wachakataji na wawekezaji wadogo kujitokeza kwa
wingi ili kupata mkopo endapo kampuni ya PASS itakuwa imeadhinisha kwa
mteja husika kupata mkopo huo.
"Wawekezaji na wakulima
wadogo msiogope kuitumia Benki ya NBC kwani ni benki yenu ambayo ipo
tayari kuwasaidia ili mtimize malengo yenu kwani wengi wamenufaika na
mikopo hiyo hadi sasa wanafanya biashaza za mazao yao hadi nje ya nchi,"
alisema.
No comments:
Post a Comment