Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Martin Shigela (kulia), akimsikiliza Meneja Kiwanda cha Kampuni ya Tanga Cement
(TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kushoto) katika hafla ya ufunguzi wa safari
za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini
Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano
na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor na Mkuu wa Wilaya ya
Rombo, Agnes Hokororo.
Meneja Rasilimali watu
wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi akishikana mikono na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa (kulia)
wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar-
Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa
wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga
Cement, Bi. Mtanga Noor, Meneja Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema na
Meneja Mauzo Taifa wa kampuni hiyo, Leslie Massawe.
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa (kulia) akishikana mikono na
Meneja Mauzo Taifa wa kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Leslie Massawe wakati wa
hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga-
Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine
kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi.
Mtanga Noor, Meneja Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema, Meneja Rasilimali
watu wa Kampuni ya Tanga Cement, Diana Malambugi na Meneja Biashara wa Kampuni
hiyo, Peet Brits.
Meneja Kiwanda cha
Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi
wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika
mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa (katikati) akipunga mkono kwa baadhi ya wakazi na mashuhuda wengine
waliofika katika uzinduzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar-
Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wakazi wa
Moshi na wananchi wengine wakiangalia treni la kwanza la mizigo lililobeba
saruji ya Tanga Cement baada ya kuwasili katika stesheni ya Moshi wakati
wa uzinduzi wa safari za treni hiyo litakalofanya safari zake katika reli ya
Dar- Tanga- Kilimanjaro. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Moshi, Kilimanjaro
mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi
wa Kampuni ya Tanga (TCPLC) pamoja na washuhudiaji wengine wakihudhuria
uzinduzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar - Tanga - Kilimanjaro
uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi
alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Uzinduzi
wa reli ya Tanga - Moshi utaongeza kipato kwa mikoa ya kaskazini
Na Mwandishi wetu, Moshi
Uzinduzi wa huduma za reli kati ya
Tanga na Moshi utaongeza kipato kwa mikoa miwili hiyo, kuchagiza kukua kwa
sekta ya ujenzi majumba na zaidi kuifanya Tanga ijitwalie hadhi
yake ya zamani enzi za kilele cha zao la katani katika soko la dunia,
ambapo Tanga ulikuwa ni mji maarufu, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga
Cement Reinhardt Swart akiongea kuhusu uzuduzi huo.
Kampuni ya Tanga Cement ilikuwa ni mteja wa kwanza wa
huduma hizo mpya ambazo zilisita miaka 12 iliyopita, ambapo treni hiyo
iliwasili katika stesheni ya treni ya moshi mjini ikikokota mabehewa
yaliyosheheni jumla ya tani 800 kwa mpigo, mzigo ambao ni swan a ule ambao
ungesafirishwa na malori 30.
“Ninaamini usafirishaji kwa urahisi wa bidhaa kati ya
vituo hivyo viwili utaongeza kiwango cha watu kuzalisha kipato kwa mikoa yote
miwili. Sisi tunahitaji watu wengi zaidi wajipatie pesa mifukoniu mwao ambayo
itawasaidia kujenga nyumba bors ambazo bila shaka zinahitaji aruji, hivyo tutaongeza
mauzo yetu, kuonheza kipato cha wanahisa wetu kupitia gawio, serikali ya
Tanzania itavuna kodi ambayo itasaidia katika maendeleo ya nchi,” alisema
mkurugenzi huo.
Aliongeza kuwa Tanga ni eneo muhimu la kiuchumi na ina
miundombinu yote muhimu ambayo ni bandari, barabara na reli. Wahusika
wakivisimamia hii miundombinu vyema na kuitumia ipasavyo, alisema ana uhakika
kuwa ‘ baada ya mika michache, tanga itakuwa zaidi ya ilivyokuwa enzi
zake za kilele cha katani, kitu kilichofanya Tanga uwe ni mji maarufu
nchini Tanzania na Afrika Mashariki.
Kampuni ya Tanga Cement ni kati ya wateja wakubwa wa Kampuni ya
Reli Tanzania (TRC) na mwaka 2016 illisaini mkataba wa iliyokuwa TRL kuwezesha
usafirishaji wa saruji kutoka Tanga Cement kuwaendea wateja wa kampuni hiyo
waliopo mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Mkataba huo wa makubaliano ulitiwa saini ili kuwezesha
usafirishaji wa zaidi ya tani 35,000 za saruji kwa mwezi. Kampuni ya Tanga
cement ilitengewa vichwa vitano vya treni na kichwa cha treni cha kupangia
mabehewa ili kuwezesha usafirishaji watani 20,000 kwa mwezi kutoka Ponge hadi
kigoma, na tani 15,000 kwenda mwanza.
“Hii ilikuwa ni hatua muhimu ya mafanikio katika kupatia
ufumbuzi usafirishaji wa saruji. Tumejenga uhusiano mzuri sana na TRC ambapo
tunakutana mara kwa mara kuhakikisha kuwa kila jambo linakwenda sawia
hasa kuhusiana na utekelezaji wa mkataba huo wa makubaliano na tunatoa
mapendekezo yanapohitajika na kushauri marekebisho ya hapa na pale, aliongeza
Ndugu Swart.
Kukua kwa ujenzi wa mjumba mbao mkurugezi huyo wa Tanga cement
anautabiri siyo ndoto ya alinacha, kwa kuwa wadau wanakubaliana
kuwa matumizi ya reli katika kusafirisha saruji kutapunguza gharama za
usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa ujenzi, na hivyo kusababisha bei ya
saruji kushuka.
Akiongea katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa alisema kuwa wachambuzi wa kimataifa wanakadiria kuwa kutumia reli
badala ya barabara kunapunguza gharama za usafirishaji kwa kiwango cha
asilimia 30-40.
Kwa mujibu wa wadau wa sekta ya usafirishaji, kusafirisha tani moja
ya saruji kutoka Tanga hadi Moshi kwa barabara kunagharimu Tsh 40,000, wakati
reli inakadiriwa kugharimu Tsh 28,000. Tanga Cement yenyewe inatarajia
kusafirisha jumla ya tani 1,600 kwa wiki na 80,000 kwa mwaka kutoka kiwandani
Tanga hadi Moshi.
Waziri Mkuu Majaliwa Alisema “Usafiri wa reli ni kichocheo
kikubwa cha ukuaji wa uchumi nchini, kwa kutumia reli, inawezekana
kusafirisha bidhaa nyingi kwa wakati moja. Nina hamu ya kuona kuwa watu
wanatumia fursa hii ya huduma ya reli kuagiza bidhaa, na bila shaka bei ya
bidhaa itapungua”
Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mwenyekiti wa Bodi wa
TRC Prof. Kondoro, naye alichangia swala la reli kupunguza gharama, na akasema
kuwa kuziduliwa kwa huduma za reli kati ya Tanga na Moshi ni sehemu ya mkakati
wa serikali na TRC kuhakikisha kuwa gharama za usafirishaji wa bidhaa
zinapungua, kama njia ya kusaidia kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Alisema Prof. Kondoro “Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati
madhubuti wa kuona kwamba tunasafirisha bidhaa kwa gharama nafuu, na kwa kuwa
kutumia reli kunapunguza gharama za usafirishaji, hii itasababisha bei za
bidhaa kushuka sokoni.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa TRC Masanja Kadoigosa, kwa mara
ya mwisho treni ya mizigo kwenda Moshi kutokea Tanga, umbai wa km 438, ilikuwa
mwaka 1993, huku treni ya abiria ikisitisha safari zake mwaka 1994.
Ujenzi upya wa reli ya Tanga – Moshi ulianza mwaka
2017 na kukamilika mwaka 2019, na ulijumuisha wafanyakazi 525, wahandisi 12,
vibarua 466 na wafanyakazi maalum 47, huku mitambo zaidi ya 43 ya aina
mbalimbali ikitumika, alisema Kadogosa.
Mtandao wa reli Tanzania umetambaa juu ya jumla ya maili 2707,
ukipita juu ya madaraja zaidi ya 3,000 na vituo 126, alisema mkurugenzi
huyo wa TRC ndugu Kadogosa.
No comments:
Post a Comment