Na Mwandishi Wetu,
BENKI ya NBC imewahakikishia wateja na
wananchi kwa ujumla kuwa mtandao wa mawakala wake unazidi kuongezeka sehemu
mbalimbali nchini kote huku wakizidi kuboresha huduma za NBC Wakala ili
kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na zinazokidhi mahitaji yao.
Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na
benki hiyo kwa Mawakala wake zaidi ya 600 jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema pamoja na kuboresha mtandao
wa mawakala benki imeendelea pia kuboresha mtandao wake wa kidigitali, ATM na
matawi yao yaliyotapakaa sehemu mbalimbali nchini.
Akizungumzia kuhusu semina mawakala Bwana
Sabi alisema, semina hiyo pamoja na kwamba ni matakwa ya ya kisheria ya Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), bali pia wanapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara
na kuzungumza jinsi biashara inavyokwenda, maeneo ya kuboresha, changamoto
zinazowakabili na kuona jinsi benki inavyoweza kuzitatua.
“Tumezungumza mengi, lakini zaidi ni fursa
kwa walaji wa mwisho za huduma za kibenki, tumeweza kuwaeleza mawakala juu ya
huduma za benki na jinsi mtandao huu wa mawakala unaokuwa kwa kasi
unavyoimarika, na pia ambavyo tunaendelea kuboresha huduma zetu.
“Utaratibu huu utaendelea japo mara mbili
kila mwaka ili kuhakikisha tunakuwa karibu sana na wenzetu hawa mawakala ambao ni muhimu sana kwetu katika kuhakikisha walaji wa mwisho wa huduma zetu wanapata
huduma zilizo bora na zinazokidhi mahitaji yao,” aliongeza mkurugenzi huyo.
Naye Mkuu wa Huduma
za Benki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha
alisema NBC Wakala iliyoanza Mwezi June, 2018 na kufikisha mawakala zaidi ya
1800 ni moja ya mkakati wa benk hiyo katika kuunga mkono azma ya serikali
katika kuhakikisha wananchi walio wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.
“Tumekutana hapa ili kufahamu kutoka kwao
yale yanayojiri katika maeneo wanayofanyia biashara na pia kuwajengea uwezo na
elimu ya utoaji wa huduma za kibenki sambamba na kanuni za sheria ya utoaji wa
huduma za kibenki inavyotaka tufanye,” alisema.
Pamoja na hayo alisema NBC ipo mbioni katika
kuhakikisha kuwa huduma zao nyingi zinapatikana kupitia mawakala kama kufungua
akaunti za papo hapo (fasta akaunti), vituo vya kukusanya taarifa za miamala, huduma
za mikopo, bima, taarifa za ubadilishaji wa fedha za kigeni, na pia wateja
kuwasilisha malalamiko na maoni kuhusu huduma za NBC tofauti na ilivyo sasa
ambapo huduma hizo hupatikana katika matawi pekee.
“NBC inayo malengo kuwa ifikapo Mwaka 2020
sehemu kubwa ya huduma zinazopatikana kwenye matawi ziweze kupatikana kupitia
mawakala wao na hiyo itawasaidia pia katika kuwaongezea kipato,” aliongeza
Bwana Mosha.
Mmoja wa Mawakala waliohudhuria semina hiyo, Mama
Tumaini Bureta wa Mikocheni, Dar es Salaam alitoa pongezi kwa NBC akisema amejifunza
mengi hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki hivyo ana matumaini mrejesho
waliotoa kwa NBC ukitekelezwa unaweza kuboresha huduma wazitoazo na wao
kufaidika kwa sehemu kubwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na baadhi ya mawakala wa
benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za
kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi
karibuni.
Mkuu
wa huduma za benki kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha, akizungumza na
baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya
utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar
es Salaam hivi karibuni.
Meneja Ukuzaji wa Biashara wa Kitengo cha
biashara ndogondogo na za kati wa Benki ya Taifa ya Biashara, Jonathan
Bitababaje, akizungumza na baadhi ya
mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa
huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na baadhi ya mawakala wa
benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za
kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam
hivi karibuni. Pamoja naye ni baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo.
Mkuu
wa huduma za benki kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha (kushoto),
akikabidhi cheti kwa mmoja wa mawakala wao Monica Kikoti baada ya kuhudhuria
semina kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa
na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi
ya Mawakala wa Benki ya NBC wakihudhuria semina iliyoandaliwa na benki hiyo juu
ya utoaji wa huduma za kifedha kupitia NBC Wakala, jijini hivi karibuni.
Mnadhimu
Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NBC, Joyce Mbago (kushoto),
akikabidhi cheti cha wakala wa benki hiyo Dianarose Buddybruno katika
semina kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala hao iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Hongereni NBC mnafanya kitu kizuri
ReplyDelete