Nabii Nicolaus Suguye akisaini moja ya Kitambaa cha muumini wa Kanisa hilo
Na Mwandishi wetu,
KATIKA jambo
lililowashangaza wengi, ndani ya Kanisa la WRM lillopo Kivule Matembele ya
Pili, Ukonga, jijini Dar es Salaam, Kiongozi na Msimamizi Mkuu wa huduma hiyo,
Nabii Nicolaus Suguye ameendesha Ibada ya kutia saini vitambaa vya maelfu ya
waumini wa kanisa hilo.
Neno saini
limetoholewa kutoka katika neno la kiingereza ‘sign’ ili lifanane na muundo wa
Kiswahili na liwe ni neno kamili la Kiswahili na kutumika kama kitenzi na
wakati mwengine kama nomino.
Nabii Suguye akionesha dhamiri ya dhati kuhakikisha kila aliyehudhuria Ibada hiyo anamsainia kitambaa chake.
Saini
(kitenzi) ni kutoa idhini ili kitendo Fulani kitendeke au kipatikane. Matumizi
yaliyozoeleka na kukubaliwa na wengi ni kutoa idhini au kuthibitisha kupatikana
kwa kitu au jambo Fulani na mara nyinine ni kwa kuandika jina lako.
Tunatumia neno
hili tunapotaka kuweka saini mahali fulani. Ni sahihi kusema kuweka saini na
wala siyo kutia saini. Kutia lina maana ya kufanya kitu kiwemo ndani ya kitu
kwa mfano nitilie chai badala ya kusema niwekee chai. Kuweka kitu maana yake ni
kukitua kitu kama vile kuweka kitabu mezani au kuweka silaha chini.
Msururu wa Waumini ukisubiria kusainiwa Leso zao na Nabii Suguye
Neno sahihi
(nomino) lina maana ya kuthibitisha au kuidhinisha kwa jambo kutendeka au
kupatikana.
Awali nabii Suguye aliwafundisha maelfu ya waumini wa
kanisa hilo umuhimu wa kuthibitishwa na Mungu, “Unapothibitishwa ni rahisi
kwako kuomba lolote kwa Yule aliyekuthibitisha na akalifanya”
“Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu,
nitalifanya.” Nabii alinukuu kutoka kwenye maandiko ya Biblia
Injili ya Yohana 14:14
“Ninaposaini Leso ya kila mtu aliye hudhulia mahali hapa hii ni Saini ya USHINDI,
ninapoisaini mahali hapa imesainiwa mbinguni na kupitishwa kuwa MSHINDI”
alisema Nabii Suguye.
Nabii Suguye akiwahubiria maelfu ya waumini waliohudhuria Ibada hiyo
Akifundisha katika Ibada hiyo alisema kupitia tendo hilo
la Imani iwe ni fahari kwao kujua kuwa, kuna umuhimu wa kujitakasa na kuwa
katika mstari ule Neno la Mungu linatufundisha ili tupate kuthibitishwa nakuwa
na hakika ya kupokea yale yote tuyaombayo kwa Mungu.
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Waebrania 11:1
“Kupitia saini hii
nakutabiria ukafanikiwe katika kila kitu utakachokwenda kukifanya kwaajili ya
Utukufu wa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo.” Alisema Nabii Suguye wakati wa
Ibada hiyo.




No comments:
Post a Comment