Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda (kulia) akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala. (Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi TV)
Mafundi wakiendi kazi ya ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi TV)
Muonekano wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi TV)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam, Paul Makonda akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Barabara
ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam, inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo
amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza
kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala. (Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi TV)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala. (Picha na Brian Peter)
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua Maendeleo
ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala inayogharimu zaidi ya
Shilingi Bilioni 200 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili
mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.
RC
Makonda amesema kwa muda mrefu wakazi wa Mbagala walikuwa wakipata changamoto
ya usafiri ikiwemo foleni na wakati mwingine wananchi kuibiwa simu na mikoba
wakiwa wanagombania usafiri lakini kukamilika kwa mradi huo itakuwa mwarobaini
wa kero zote zilizokuwa zikiwasumbua.
Aidha
RC Makonda amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafanya Barabara ya Kilwa
kuwa na Njia sita, Madaraja Mawili Makubwa na Flyover jambo litakalosaidia
kurahisisha shughuli za usafiri.
Aidha
RC Makonda amezungumzia changamoto ya Mafuriko Mto Msimbazi kujaa eneo la
Jangwani na kusababisha kusimama kwa shughuli za usafiri ambapo amesema
Serikali ipo katika hatua ya kuanza kwa maboresho ya eneo hilo ikiwa ni pamoja
na kuinua Daraja na kufanya mto msimbazi kuwa sehemu ya utalii wa Boti ambapo
ujenzi unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 200.
Kuhusu
Ugonjwa wa Corona, RC Makonda amesema tayari amewaelekeza Wakuu wa Wilaya
kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu ya kuwahifadhi watu wote wanaotoka nje ya
Nchi (karantini) ili wakae chini ya uangalizi kwa muda wa siku 14 huku
akiwahimiza wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya Virusi hivyo vya
Corona.

No comments:
Post a Comment