Kampuni Ya Vodacom Tanzania PLC Yakinga Wateja Wake Waendapo Kupata Huduma Vodashop - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, April 29, 2020

Kampuni Ya Vodacom Tanzania PLC Yakinga Wateja Wake Waendapo Kupata Huduma Vodashop

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akimkabidhi zawadi ya simu mteja wa  Vodacom Abutwalib Mtua alipotembelea duka la kampuni hiyo lililopo makao makuu, kuangalia namna watoa huduma wanavyowalinda Wateja wao kipindi hiki cha janga la Corona kwa kusisitiza uvaaji wa barakoa, kuwapima joto na kuwapa vitakasa mikono mara waingiapo kupata huduma kwenye maduka ya kampuni hiyo. Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia na Mkuu wa Idara ya Uhusiano, Jacquiline Materu.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akimkabidhi zawadi ya Power Bank mteja wa Vodacom, Naseeb Shaban alipotembelea duka la kampuni hiyo lililopo makao makuu kuangalia namna watoa huduma wanavyowalinda Wateja wao kipindi hiki cha janga la Corona kwa kusisitiza uvaaji wa barakoa, kuwapima joto na kuwapa vitakasa mikono mara waingiapo kupata huduma kwenye maduka ya kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano, Jacquiline Materu.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akipimwa joto na Askari wa ulinzi wa Duka la Vodacom, Masafa Hamad Muba hii ni namna mojawapo ya kampuni hiyo inavyowalinda wateja wake katika kipindi hiki cha janga la Corona kwa kusisitiza uvaaji wa barakoa, kuwapima joto na kuwapa vitakasa mikono mara waingiapo kupata huduma kwenye maduka ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akimkabidhi zawadi ya Power Bank mteja wa Vodacom, Ruth Samuel Mkuchu  alipotembelea duka la kampuni hiyo lililopo makao makuu kuangalia namna watoa huduma wanavyowalinda Wateja wao kipindi hiki cha janga la Corona kwa kusisitiza uvaaji wa barakoa, kuwapima joto na kuwapa vitakasa mikono mara waingiapo kupata huduma kwenye maduka ya kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages