RC MAKONDA APATIWA SHEHENA YA KEMIKALI KWAAJILI YA KUTENGENEZA VITAKASA MIKONO (SANITIZER) ZITAKAZOUZWA KWA WANANCHI KWA BEI NAFUU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, April 18, 2020

RC MAKONDA APATIWA SHEHENA YA KEMIKALI KWAAJILI YA KUTENGENEZA VITAKASA MIKONO (SANITIZER) ZITAKAZOUZWA KWA WANANCHI KWA BEI NAFUU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akipokea shehena ya Kemikali kwa kwaajili yakutengenezea Vitakasa mikono ili  kupunguza mfumko wa bei ya Vitakasa Mikono (Sanitizer) ili kila mwananchi aweze kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu hasa katika kipindi hichi cha kupambana na Corona.
Kaimu Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji  akizungumza wakati akimkabidhi shehena ya Kemikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwaajili yakutengenezea Vitakasa mikono ili  kupunguza mfumko wa bei ya Vitakasa Mikono (Sanitizer) ili kila mwananchi aweze kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu hasa katika kipindi hichi cha kupambana na Corona.

Mkemia Mkuu wa Serikali Fidelis Mafumiko akizungumza wakati akimkabidhi shehena ya Kemikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwaajili yakutengenezea Vitakasa mikono ili  kupunguza mfumko wa bei ya Vitakasa Mikono (Sanitizer) ili kila mwananchi aweze kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu hasa katika kipindi hichi cha kupambana na Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa shehena ya Kemikali yenye ujazo wa Lita Laki moja na Sabini 170,000 kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwaajili ya Kutengeneza Vitakasa Mikono (Sanitizer) zitakazouzwa kwa punguzo la bei la 40% ili kumuwezesha kila mwananchi anaweza kumudu gharama na kujikinga na Corona.


RC Makonda amesema kemikali hizo zitatolewa kwenye viwanda vyote vinavyotengeneza Sanitizer vilivyosajiliwa na Serikali na vyenye utaratibu wa kuuza bidhaa zao kwa Bohari kuu ya Dawa MSD ambapo amesema atavielekeza Vyombo vya Ulinzi kupita na Kudhibiti kupanda kwa bei ya Sanitizer hizo.

Aidha RC Makonda ameelekeza kila Familia ikae kikao cha dharura ili wajiwekee mkakati na mbinu za kukabiliana na janga la Corona kuanzia ngazi ya familia huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari na kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.

Kwa upande wake Kaimu Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji amesema Kemikali hizo zilikamatwa na kutaifishwa na Serikali baada ya Kushinda kesi hivyo wameona ni vyema sasa kemikali hiyo ikatumika kupunguza mfumko wa bei ya Vitakasa Mikono (Sanitizer) ili kila mwananchi aweze kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages