MUHIMBILI YAKABIDHI VAZI MALUM LA PPE KWA KAMATI ZA DHARURA KUKABILIANA NA CORONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, April 21, 2020

MUHIMBILI YAKABIDHI VAZI MALUM LA PPE KWA KAMATI ZA DHARURA KUKABILIANA NA CORONA


Na Sophia Mtakasimba & Angela Mndolwa

Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanza kusambaza  mavazi maalumu (coverall) ambayo ni sehemu ya mavazi ya watoa huduma (PPE) kuvaa ili kujikinga wakati wanatoa huduma wagonjwa wenye maambuki mbalimbali ikiwemo Covid 19 kwa kamati za dharura za Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Zuhura Mawona  alisema kuwa baada ya kujadiliana na Serikali bei elekezi itakuwa Tzs. 50,000 kwa kila vazi moja.

Manispaa ya Kinondoni imenunua mavazi 15 yenye thamani ya Tzs. 750,000, Ilala mavazi 20 yenye thamani ya Tzs. 1,000,000 huku Manispaa nyingine zikiendelea kulipia ili kupata mavazi hayo.

"Kwa sasa tunaanza na vituo vilivyopo katika Manispaa za jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine itafuata" alisema Bi. Mawona

Alisema kuwa mahitaji ni makubwa katika mikoa mbalimbali hivyo kwa sasa Muhimbili imejikita katika kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji.

Mapema wiki iliyopita Muhimbili ilizindua vazi hilo maalumu liloshonwa na wataalamu wa MNH kwa kutumia malighafi za ndani ya nchi lengo ikiwa ni kukabiliana na upungufu wa bidhaa hizo duniani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages