Na Saidat Msabaha, Dar es Salaam
Scrub ni aina mojawapo ya urembo japokuwa unaweza kufanywa kwa jinsia zote, mwanamke na mwanaume.
Zipo aina nyingi za Scrub na aina zote hizo zinalenga jambo moja tu la kufanya ngozi iwe katika hali nzuri, na hasa kuifanya ngozi kuwa huru ili kuweza kupumua vizuri na kumuhepusha mtumiaji na Magonjwa ya ngozi Kama vile kutokwa na chunusi, mapele n.k.
Scrub ya kahawa, hii ni aina nyingine ya Scrub inayoweza kuwa suluhisho sahihi kwa ngozi iliyochakaa kiasi kikubwa kwa kuondoa chunusi zilizoota mizizi, ngozi iliyofubaa, kuchoka na kukosa muonekano mzuri.
Namna ya kutumia Scrub ya kahawa, kwanza uso usiwe na makeup yoyote , unatakiwa kuosha uso wako kwa maji ya moto kwa mtu mwenye ngozi kavu, au maji ya baridi kwa mtu mwenye ngozi yenye mafuta.
Kwa mtu mwenye ngozi yenye mafuta hashauriwi kutumia maji ya moto kabla ya kutumia Scrub ya kahawa, na hata baada kutumia pia, hii ni kutokana na uhalisia wa ngozi yake tayari ina mafuta hivyo kwa kutumia maji ya moto kunaweza kusababisha Scrub kutofanya kazi kwa jinsi inavyotakiwa.
Scrub hii ni kwaajili ya wanawake na wanaume, haina kemikali yoyote wala viambata sumu.
Inashauriwa mtu kufanya Scrub angalau kila baada ya wiki mbili ili kuondoa mafuta, uchafu na 'nongo' iliyopo kwenye ngozi.
Bi Saidat Msabaha ni mtaalam wa masuala ya urembo na pia ni mtengenezaji wa bidhaa mbalimbali za urembo ikiwemo Scrub ya kahawa.
Kwa mujibu wa wataalamu, ngozi huwa ina haribika pale inapoachwa kwa muda mrefu bila kupewa matunzo hasa kutofanyiwa Scrub kwa wakati na kwa usahihi na hivyo kunaweza kusababisha madhara makubwa.
Kuna umuhimu mkubwa watu wa Jinsia zote kufanya Scrub.
"Kuna umuhimu mkubwa wa mtu kufanya Scrub, mara nyingi uso unakuwa na uchafu ambao huwezi kuuona kwa macho na ule uchafu unaenda kuziba vinyweleo na kufanya ngozi ishindwe kupumua vizuri na matokeo yake kumfanya mtu aanze kutokwa na chunusi nyingi na mapele makubwa usoni" Alisema Saidat.
No comments:
Post a Comment