Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa dini kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini katika Mkutano uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea jinsi Wizara inavyoshirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkutano kati ya Wizara (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Gilbert Kamanga akielezea jinsi Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkutano kati ya Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa kidini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika Mkutano kati yao na Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu amesema Tanzania imeanza kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ya
ndani kuanzia maambukizi yaliyopatikana tarehe 08/04/2020.
Amesema kuwa tahadhari kubwa inahitajika katika kuhakikisha kuzuia kuendelea
kwa maambukizi ya kijamii itasababisha kuongezekana kwa kasi ya maambukizi
katika jamii.
Ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na
viongozi wakuu wa madhehebu ya dini katika kujadiliana namna ya kukabiliana na
maambukizi ya virusi ya Corona nchini.
Ameongeza kuwa Serikali itatangaza hivi karibuni wananchi kuchukua
tahadhari kwani tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaweza kusambaa na
kuambukizwa kwa njia ya hewa hivyo maelekezo ya kutumia barakoa yatatolewa ili
kuondokana na maambukizi.
“Tafiti zimeonesha kuna uwezekano wa Virusi vya Corona vinaweza
kuenezwa kwa njia ya hewa hivyo tutaleta muongozo wa kuanza kutumia Barakoa
(Mask) kwa jamii ili kuziua maambukizi kuenena kwa njia ya hewa” alisema.
Aidha amewataka viongozi wa dini kutoa rai kwa wazazi na walezi
kuwalinda watoto kutowaruhusu Watoto kuzurula na kuhangaika ovyo mitaani ili
kupunguza uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
“Imani ya watanzania wengi kufikiri kuwa hatuwezi kupata maambukizi ni
suala sahihi tunaweza kupata maambukizi kama watu wengine wanavyopata” alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema
kuwa viongozi ni watu muhimu katika kuleta mabadiliko katika Jamii yetu kwani
wanasikilizwa zaidi na waumini katika sehemu za ibada.
Ameongeza kuwa lengo ni kuwashirisha viongozi wa kidini katika
kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya
Corona yanatokomea nchini.
"Viongozi wa kidini ni watu muhimu sana katika mapambano katika kuondokana
na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini tunaomba mtusaidie katika hili"
alisema.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Gilbert Kamanga amewaomba
vingozi wa dini kutofanya suala la virusi vya Corona kuwa la kisiasa bali
waunganishe nguvu pamoja ili kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kupewa elimu kila mahali ikiwemo katika
nyumba za ibada ambapo watu wengi ukusanyika pamoja kuabudu itakuwa sehemu
sahihi kufikisha ujumbe kuhusu kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
"Viongozi wetu wa dini nawaomba tushikamane katika hili kwani
virusi vya Corona ni hatari sana lakini tukisimama pamoja hakika tutafanikiwa
katika kutokomeza virusi vya Corona" alisema.
Akitoa salam za mkoa wa Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt.
Rashid Mfaume amesema mkoa umejidhatiti katika kupambana kwa kuenea na maambukizi
ya Virusi vya Corona mkoani humo kwa kuzingatia maelekezo yanayotokea na
wataalam wa Afya na Serikali kwa ujumla.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Musa Salum amesema
janga la Corona ni kubwa na kama watu wa imani tunaamini katika kumuonba
Mwenyezi Mungu na tunaamini litatokomea.
Pia amemshukuru Rais John Magufuli kuendelea kuruhusu ibada kuendelea
katika kama kawaida ni jambo ambalo litasaidia kuzidisha maombi katika
kupambana na Virusi vya Corona.
Mkutano huu kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini umekuja wakati
Tanzania ikiendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona huku ikiwa na
jumla ya watu 25 waliombukizwa virusi hivyo.
No comments:
Post a Comment