ZANZIBAR yasimamisha MAKUTANO ya waandishi wa Habari - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 13, 2020

ZANZIBAR yasimamisha MAKUTANO ya waandishi wa Habari


Katika Kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona na kuepuka mikusanyiko , Kuanzia leo Aprili 13 mwaka 2020 Mikutano ya Waandishi wa Habari na shughuli nyengine zitakazowafanya waandishi wa habari kukusanyika zinasitishwa.

Hivyo, basi taarifa za Waziri wa Afya Zanzibar kuhusiana na Virusi vya ugonjwa wa Corona zitatolewa kwa njia ya 'Press Releases', kurusha moja kwa moja kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) au kurekodiwa na kusambaza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari na umma kwa ujumla.



Taasisi zote zenye shughuli zitakazowajumuisha waandishi wa habari tunawaomba kutumia njia tulizozieleza na kujiepusha kwa namna yoyote ile kuwaita waandishi wa habari katika shughuli zao.

Wahariri na waandishi wa habari tunawasisitiza kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na Serikali kwa ujumla kwa kuepuka mikusanyiko Dkt Juma ohammed alum Mkurugenzi Idara ya Habari.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages