TCAA yafuta SAFARI zote za NDEGE za abiria za KIMATAIFA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 13, 2020

TCAA yafuta SAFARI zote za NDEGE za abiria za KIMATAIFA


Mamlaka ya Usalama wa Anga nchini imefuta safari za ndege zote za abiria za kimataifa na kuweka vikwazo zaidi kwa ndege maalum za mizigo zitakazoruhusiwa kutua nchini. Hii ni hatua nyingine ya kupambana na Ugonjwa wa Covid-19.



Kwa mujibu wa taarifa ya TCAA, safari zote za ndege zilizokuwa zimepangwa na zile ambazo hazikuwa zimepangwa zimezuiwa hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

Licha ya zuio hilo, TCAA imebainisha kuwa ndege za mizigo zitaruhusiwa kuingia nchini, lakini wahudumu wa ndege hizo watawekwa Karantini kwa gharama zao katika maeneo yaliyotengwa na serikali kwa kipindi chote watakachokuwa nchini.

Mpaka April 13, Tanzania immeripoti visa 46 vya maambukizi ya virusi vya Corona, vifo vitatu na wagonjwa saba wamepona.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages