Mhandisi Stella Manyanya akabidhi malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 10, 2020

Mhandisi Stella Manyanya akabidhi malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amekabidhi malighafi (Ethanol) inayotumika kutengeneza vitakasa mikono (Hand Sanitizer) iliyotolewa na kiwanda cha Kilombelo Sugar Company Limited na Wizara kuchukua jukumu la kugawa malighafi hiyo kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi ya utafiti wa Teknolojia (TIRDO) pamoja na taasisi ya kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

Hii imekuja kutokana na kikao cha Tarehe 25 Machi, 2020 kilichoitishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alipokutana na wenye Viwanda vya kuzalisha malighafi zinazotumika kutengeza vitakasa mikono (Hand sanitizer). Kampuni ya Consumer choice kwa kuona umuhimu wa agizo la waziri la viwanda hivi kusaidia kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa Korona (COVID 19) Kiwanda hiki kilibeba jukumu la kusafirisha ethanol lita 30,000 zilizotolewa na Kilombero Sugar Company Limited kuzileta Dar es salaam ili kukabidhi kwa Wizara ya Afya, TIRDO na SIDO.

Pamoja na ahadi hiyo Kampuni ya Consumer Choice iliamua kubadili 75% ya ethanol iliyokuwa ikitumika kutengeza kilevi itumike kutengeza vitakasa mikono (Hand sanitizer).

Kampuni ya Consumer Choice kwa kushirikiana na kampuni ya G & Co. Limited & Sanitation Ltd na kufanikiwa kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer) Lita 11,000 zilizotokana na lita 8,000 za ethanol kati ya lita 20,000 walizopewa wizara ya afya.

Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya ameishukuru Kampuni ya Consumer Choice kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa COVID 19 kwa kuunga mkono mchango wa Kilombero Sugar kwa kugharamia gharama za usafirishaji wa malighafi hii ya ethanol kutoka kiwandani Kilombero hadi Dar es salaam.

Mhe. Manyanya amesema kuwa “Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikina na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufanya kazi usiku na mchana kupambana na janga hili kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa kinga vya kuzuia usambaaji wa ugonjwa huu vinapatikana kwa wingi”.

Mhe Manyanya ametoa wito kwa wenye viwanda vya kutengeneza vifaa kinga nchini kuongeza bidii katika uzalishaji ili kuwezesha maeneo yote ya nchi kupata vifaa hivyo kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Ameongeza kwa kusema kuwa taasisi zinazopokea malighafi kutumia malighafi hiyo kuokoa maisha ya watanzania kwa kuzalisha vitakasa mikono vyenye bei nafuu.

Aidha Mhe. Manyanya amewasihi wadau wengine wenye viwanda vyenye mifumo inayoweza kutengeneza vitakasa mikono kuweka nguvu kwenye uzalishaji wa vifaa hivi kwa wingi ili kusaidia mapambano haya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages