Mlezi Mkuu wa Kituo cha CHAKUWAMA, Hasan Hamisi akizungumza mara baada ya Taasisi ya tumaini la Mtoto kutoa elimu na kutoa vitu mbalimali katika kituo hicho kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Taasisi ya Tumaini la Mtoto, Maziku Kuwandu akiwaonesha watoto wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha CHUKUWAMA jinsi ya kunawa ili kujikinga na virusi vya Corona (COVID 19).
Mkurugenzi Taasisi ya Tumaini la Mtoto, Maziku Kuwandu na Agness Liziki wakionesha watoto jinsi ya kujitakasa mikono ili kuepukana na Virusi vya Corona (COVID 19).
Watoto wakioneshwa aina mbalimali za sabuni ya kijitakasa mikono.
Agness Maliki akitoa elimu kwa watoto wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha CHUKUWAMA kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya watoto wa kituo cha CHUKUWAMA akijibu swali.
Baadhi ya watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHUKUWAMA.
TAASISI isiyo ya kiserikali ya Tumaini la Mtoto imetoa elimu na msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha CHUKUWAMA kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Akitoa elimu kwa watoto wa kituo hicho Mkurugenzi Taasisi ya Tumaini la Mtoto, Maziku Kuwandu amesema kuwa Watoto waliopo kwenye vituo vyao vya kulelewa wamekuwa hawapati elimu ya kujikinga na Virusi vya Corona (Covid 19) ndio maana wachukua fursa hiyo kuwapa elimu watoto hao.
"Taasisi ya Tumaini la Mtoto kupitia kampeni ya nivalishe imechukua fursa ya kuwapa elimu watoto wa kituo cha CHUKUWAMA ili watoto waweze kuwa na uelewa juu ya janga la dunia pamoja na kuchukua tahadhari. " Amesema Kuwandu.
Licha ha hilo Mtoa mada mwingine Agness Maliki amewaeleza kinagaubaga na kwa vitendo namna ambavyo wanaweza kunawa mikono yao kwa sabuni na maji tiririka ili watoto hao wawe na uelewa mzuri katika kujikinga na virusi vya Corona (COVID 19).
Hata hivyo katika kutoa elimu hiyo watoto waliweza kupewa nafasi ya kunawa mikono kama walivyoelezwa na Agness.
Kwa upande wa Mlezi Mkuu wa Kituo cha CHAKUWAMA, Hasan Hamisi amewashukuru wafanyakazi wa Taasisi ya Tumaini la Mtoto kupitia Kampeini ya Nivalishe kwa kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona (COVID 19) katika kituo hicho pamoja nakutoa vitu mbalimbali.
"Mimi pamoja na watoto tunawashukuru sana Taasisi ya Tumaini la watoto kupitia kampeni ya nivalishe kwani sio kila mtu anaweza kufanya kile ambacho taasisi yenu imefanya." Amesema Hamis.
Hamis ameomba wadau mbalimbali wajitokeze katika kusaidia kituo hicho kwani kunachangamoto katika Elimu pamoja na Afya kwa watoto.
Amesema kuwa katika upande wa elimu wapo watoto wanaosoma katika shule mbalimbali na madarasa tofauti na kila mmoja anamahitaji yake hivyo kama kituo wamechukua changamoto hizo ili watoto wasio nawazazi wapate haki zao kama watoto wengine.
No comments:
Post a Comment