WAZIRI DKT KALEMANI ATAKA WANAOIBA UMEME WAKAMATWE NA KUWEKWA KOROKORONI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 10, 2020

WAZIRI DKT KALEMANI ATAKA WANAOIBA UMEME WAKAMATWE NA KUWEKWA KOROKORONI


WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika akikata utepe kuashiria kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake katika wilaya za Lushoto,Handeni na Korogwe mkoani Tanga iliyokuwa inalenga kutembelea kwenye maeneo yanayofanyiwa kazi na wakandarasi kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu unaoendelea ambao unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu kulia ni Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kweisasu Kata ya Sindeni wilayani Handeni mara baada ya kuwasha umeme katika eneo la Shule ya Msingi Kweisasu wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme kwenye moja ya nyumba zilizopo kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake kushoto anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando kulia ni mzee mwenye nyumba hiyo

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akizungumza na mzee wa nyumba aliyowasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake.

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa Meneja wa Tanesco wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Gaspar Msigwa kushoto na kulia anayefuatilia kwa umakini ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tanga Mhandisi Julius Sabu wakati alipowasilia eneo la Mkata wilayani Handeni kwa ajili ya kuanza ziara yake mkoani hapa.
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari kuhusu namna kituo cha Umeme Kilole kinavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye kituo hicho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando.
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari wakati alipotembelea kituo cha Umeme cha Kilole wilayani Korogwe wakati wa ziara yake

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameagiza watu ambao watakaobainika kuhujumu miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kuiba umeme au vifaa vyake wakamatwe na kuwekwa korokoroni ili waendelee na utaratibu wa kisheria kusudi watu wengine wenye nia mbaya wajifunze na kuachana na vitendo hivyo.

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika wilaya za Lushoto,Handeni na Korogwe mkoani Tanga iliyokuwa inalenga kutembelea kwenye maeneo yanayofanyiwa kazi na wakandarasi kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu unaoendelea ambao unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu.

Kauli ya Waziri huyo inatokana na Taarifa aliyopatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando wakati alipofika kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani humo ambapo alielezwa namna wizi wa umeme ulivyokithiri kwenye wilaya hiyo.

Licha ya kuwasha umeme kwenye baadhi ya vijiji kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe na Lushoto pia alifanya ufuatiliaji huo ili waweze kukamilisha kazi yao ndani ya muda huo na amekwisha kutoa maelekezo kwa nchi nzima kwa wakandarasi wote wanaoendelea kwa wale ambao watashindwa kumaliza kazi zao kwa mujibu wa mkataba wake ambao unaishia mwezi June mwaka huu.

Maelekezo hayo ni kwa wanaowasimamia wahandisi wote waanze kuwakata malipo yao ya mishahara kwenye mikataba hiyo ambayo ni kwa mujibu wa mikataba ya malipo hayo huku akiagiza ikikatwa wasikae nayo wairejeshwe kwa katibu mkuu hazina ambaye ni mlipaji mkuu wa serikali ili fedha hizo zitumike kwa ajili ya kuwaweka wakandarasi wengine ambao wataweza kumaliza kazi hizo.

“Ndugu zangu ikibainika mtanzania amefanya hujuma ya kuiba umeme au vifaa vyake mtu wa namna hiyo ni mhujumu achukuliwe hatua na viongozi wa maeneo husika wala suala hilo sio la kumsubiri meneja wa mkoa aje ajiridhishe tunaomba ma DC msisite kutoa taarifa…

“Lakini kwa wasiokuwa na nia njema ya miumbonu ya umeme wakamateni na wawekeni Korokoroni na muendelee na utararibu wea kishereia kusudu watu wengine wenye nia mbaya wajifunze kutoka kwenye tabia hizo ambazo sio nzuri kwa ustawi wa shirika letu kwani wanakuwa wakirudisha nyuma juhudi kubwa tunazozifanya" Alisema

Aidha Waziri Dkt Kalemani alisema wakati mwengine kunapotokea wizi mameneja nao wanakuwa sehemu ya wizi huo kama sio wao ni vibarua wao kwa sababu haiwezekani mtu ambaye haujui umeme anafungua transfoma na kuiba umeme bila kujua taalumu ya umeme halafu anaiba vifaa bila kuuungua lakini hatama kama sio mtaalamu wa tanesco ni mtu aliyewahi kufanya kazi nanyi

“Nikisiria transfoma imeibiwa mahali mtu wa kwanza kumchukulia hatua ni meneje wa eneo husika kwa sababu yeye ndio mwenye jukumu la kusimamia wataalamu wake anaowapa kazi lakini pia acheni kuwapa kazi vishoka kwani mnapowapa kazi matokeao yake ndio hayo”Alisema Waziri Dkt Kalemani.

Akizungumzia suala tatizo hilo mbele ya Waziri wa Nishati, Katibu Tawala wa wilaya hiyo Rahel Mhando alimueleza kwamba kumekuwa na tatizo la wizi wa umeme hilo tatizo bado lipo Korogwe ni kubwa huku akieleza kwamba wameweka mikakati mbalimbali kama wilaya ya kuweza kukabiliana nalo

“Mh Waziri  amekwisha kutoa maelekezo na sisi kama wilaya tumepokea maelekezo hayo na labda nisema kwamba kwa yoyote tutakayembaini anaiba umeme huo ni hujumu uchumi atachukuliwa hatua kali na hatutawatamfumbia macho hilo hazungumzia waziri tu bali hata Rais Dkt John Magufuli kila siku amekuwa aksisitiza wizi wa miundombi ya umeme na kubuka umeme hilo wataendelea kulifanyia kazi”Alisema

Hata hivyo Katibu Tawala huyo alimshukuru Waziri kwa kufika kwenye kijiji cha Kwasunga kuwawashia umeme ambacho kina kaya 204 ambazo zimekwisha kupata umeme lakini kwa furaha wanamshukuru kwani mbali na vijiji vya awali zimeongezwa vijiji tisa kwenye Jimbo la Korogwe Vijiji.

“Sisi kama wilaya tunashukuru kwa sababu mmeendelea kutuongezea ukubwa upatikana umeme Korogwe kwani tuna kituo cha kilole ambacho waziri ametembelea kuna 
megawatts 5 zitaenda kuongezeka hivyo kitaongeza wigo mkubwa kwenye matumizi ya umeme”Alisema Das Rahel.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages