SADC: NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAPENDEKEZA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA MIPAKANI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, May 28, 2020

SADC: NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAPENDEKEZA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA MIPAKANI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Mkatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wa kwanza meza kuu kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya (Video Conference) Jijini Dar es Salaam.

Maafisa Waandamizi/ Makatibu Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamependekeza kuruhusu Biashara za bidhaa zote kuendelea kusafirishwa katika Nchi zao kama ilivyokuwa kabla ya janga la Virusi vya Corona.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Mkatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu amesema mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya kuondoa vikwazo vyote vya kibiashara ili kuweza kuendeleza uchumi ndani ya Jumuiya.

Balozi Ibuge amesema kuwa uamuzi huo utawawezesha wananchi kuendelea na maisha yao ya kawaida na biashara zao kwa kuwa janga la COVID 19 litaendelea kuwepo kwa muda ambao ukomo wake haujulikani japo juhudi za kuukabili ugonjwa huo zinaendelea.

“Kikao cha makatibu cha makatibu wakuu cha leo, kimependekeza kuondoa kikwazo cha bidhaa mahususi tu kupita katika mipaka yetu badala yake bidhaa zote zinazowezesha wananchi wetu kuendelea na maisha ni lazima ziruhusiwe kupita katika mipaka ya nchi wanachama wa SADC” Amesema Balozi Ibuge.

Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa ni muhimu wa wanaSADC kujumuika katika wakati huu na kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi wanachama wa SADC unakua kwa kuongeza juhudi katika sekta ya biashara.

Balozi Ibuge ameongeza kuwa “kwa mfano halisi sisi kama Tanzania hatukufunga mipaka yetu, na katika kutokufunga mipaka yetu bado tunatambua kwamba tunaendelea kuwategemea wenzetu kama wanavyotutegemea sisi…………tuna badari inayohudumia nchi nane za SADC na zisizokuwa za SADC na ambazo ndizo hasa tunapozungumzia utengamano na mazingiara ya kufanya biashara na kuzingataia tahadhari mbalimbali za uonjwa wa COVID 19 ambazo nchi hizo zimekuwa zikichukua”.

Aidha, Mkutano huu pia umejadili hali ya kifedha ndani ya Jumuiya, Utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni Menejimenti ya Maafa, utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo “Mazingira Wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC”na mapitio ya hali halisi ya biashara baina ya nchi.

Maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na Mpango kazi wake.

Mkutano huo umahusisha wataalamu kutoka nchi wanachama 12 wa SADC kutoka sekta za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha na Mipango, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Maliasili na Utalii pamoja na Afya. Mkutano huo pia utatoka na maazimio ambayo nchi wanachama watatakiwa kuyatekeleza ndani ya muda utakaokubaliwa.

Nchi zilizoshiriki Mkutano huo ni pamoja na Angola, Afrika Kusini, Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages