WILAYA YA MONDULI YAPOKEA MICHE 500 YA MITI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, May 30, 2020

WILAYA YA MONDULI YAPOKEA MICHE 500 YA MITI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Mkurugenzi wa Monduli Steven Ulaya akikabidhi miche ya miti kwa Afisa Misitu wilaya ya Monduli kama inavyoonekana katika picha.

Na Vero Ignatus, Monduli

Mamlaka ya Misitu wilaya ya Monduli (TFS) imekabidhiwa Miche ya miti zaidi 500 ili kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka Mradi wa Tunandoto Tanzania Ulio chini ya Kanisa la FPCT.

Akikabidhi miti hiyo Mkurugenzi wa wilaya hiyo Stephen Ulaya amesema amekabidhi miche hiyo kwa Mamlaka ya Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Monduli ili kuelekeza miche hiyo katika maeneo yenye uhitaji ndani ya wilaya hiyo.

Ulaya amesema miche hiyo ya Miti wamepokea kutoka Mradi wa Tunandoto ulio chini ya Kanisa la FPCT Tanzania linalo husika na Utunzaji wa Mazingira na uwezeshaji wa kaya katika Uchumi kwa kutoa elimu na Mafunzo ya Kilimo yenye tija.

Akizungumza Mara baada ya kupokea miche hiyo moja ya viongozi wa TFS wilayani humo Godlisten Koka amesema wanashukuru kwa kupokea miche hiyo na watapeleka miche hiyo katika maeneo yaliyo athirika na Mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Julius Rukyaa Mwenyekiti wa Mradi wa Tunandoto ulio chini ya (FPCT) Tanzania amesema mradi huo umekuwa ukijishughulisha na utoaji wa elimu kuhusu kilimo chenye tija katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Hata hivyo Rukya amesema tangu mradi huo umeanza zaidi ya Wananchi 1000 ikiwemo wananchi wa Monduli wamesha pata mafunzo kilimo chenye tija huku zaidi ya kaya 100 wamesha pata Mafunzo ya kujikwamua na umasikini.

Wakati huohuo Kanisa hilo FPCT kupitia mradi wake wa Tunandoto wameweza kukabidhi miche zaidi ya 500 kwa Mkuu wa wilaya ya Longido kwaajili ya kukomesha ukame katika eneo hilo na kufanya hivyo itasaidia kufanya Tanzania ya kijani

Akizungmza kwa niaba ya Mkuu huyo wa wilaya Afisa Utawala wa wilaya hiyo Malaki Tatein amesema miti hiyo wataigawa kwa wanafunzi ili kuiotesha katika maeneo ya wazi,amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukamilisha mradi wa maji mwaka jana uliogharimu Bilioni 16 ambao pia umesaidia upatikanaji wa maji yatakayo saidia umwagiliaji wa miti hiyo na kuitunza.

Aidha Mratibu wa Mradi huo Lomayani Laizer amesema mpaka sasa wamefanikiwa kugawa miti katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Arumeru,Monduli na sasa Longido ikiwa ni utekelezaji wa Mradi huo katika Shughuli zake.

Kwa Mujibu wa shirika la Mazingira Duniani UNEP limebainisha kuwa Miaka 2000 ijayo Dunia inatarajia kuwa jangwa endapo jitihada za kupanda miti hazitachukua hatamu kama ambavyo imekuwa ikifanywa na Mamlaka mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages