Tuesday, June 30, 2020

Mtego wa TAKUKURU wanasa wana CCM, watumishi, wafanyabiashara!
Na David John, TimesMajira
WATU tisa wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kwa tuhuma mbalimbali za rushwa.
Taarifa ya TAKUKURU Mkoa wa Arusha iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, James Ruge imesema kuwa, watu hao wamekamata kwa nyakati tofauti ambapo wapo pia watumishi wa Serikali na wafanyabiashara.
Imewataja watu hao wanaotuhumiwa kwa rushwa ni Sifael Palangyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi (CCM), Upendo Ndorosi ambaye ni Katibu wa Malezi Wilaya ya Longido na Mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa wa Arusha na Laraposho Laizer ambaye ni Katibu wa Wazazi Wilaya ya Longido.
Wengine ni Godwait Mungure ambaye ni Katibu wa Wazazi Kata ya Kikatiti Meru, Mboiyo Mollel ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Tukusi Kata ya Loksare wilayani Monduli,Mikidadi Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo Kijiji cha Tukusi, Kanankira Mnyari ambaye ni Wakala wa pembejeo za kilimo kijiji cha Loit kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Gervas Mollel mfanyabiashara wa Kata ya Oltrumet wilayani Arumeru pamoja na Joseph Christopher Mollel mfanyabiashara katika Kata ya Oltrumet.
Kuhusu makosa wanayotuhumiwa nayo, taarifa hiyo ya TAKUKURU imefafanua kuwa Juni 26, mwaka huu ilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa, Lilian Ntoro ambaye anatarajia kugombea ubunge wa Viti Maalum Wazazi Mkoa wa Arusha alikuwa amempatia fedha Sifael Pallangyo kwa ajili ya kwenda kuwahonga wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi Walaya ya Longido ili kushawishi kumpigia kura katika kura za maoni.
“Baada ya kupokea taarifa hiyo TAKUKURU Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Longido waliandaa mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kila mmoja akiwa na kiasi tofauti cha fedha zilizokuwa zimeandaliwa kugawiwa kwa wajumbe wa baraza la wazazi jumuiya ya Wilaya ya Longido,”imeeleza taarifa hiyo.
Pia taarifa hiyo imeeleza katika kosa la pili TAKUKURU inawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Gervas Andrea Mollel na Joseph Christopher Mollel wote ni wafanyabiashara wa Kata ya Oltrumet kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu sh.milioni 15 kutoka kwa mfanyabiashara mwenzao Advera Kyaruz mkazi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
JESHI LA POLISI LABAINI CHANZO CHA AJALI YA BASI LA PRESDAA, LAFUTA LESENI YA DEREVA
Older Article
RC MBEYA ataka UTARATIBU kuzuia MAGARI katika MITEREMKO!
Ni miaka minne ya neema kwa Mashirika ya Umma
Hassani MakeroMar 21, 2025INEC YATOA UFAFANUZI WANAOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA DAR
Hassani MakeroMar 20, 2025RAIS DKT. SAMIA ACHANGIA SH. MILIONI 50 KUMUENZI PADRI SHIRIMA
Hassani MakeroMar 20, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment