DK SHEIN AAGA RASMI ZANZIBAR NA KUWATAKA WANANCHI KUWA NA USHIRIKIANO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, July 31, 2020

DK SHEIN AAGA RASMI ZANZIBAR NA KUWATAKA WANANCHI KUWA NA USHIRIKIANO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza katika Baraza la Eid, lililofanyika Bumbwini, Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Dkt. Shein ametumia sherehe hizo kuaga rasmi wananchi wa Zanzibar.
Msafara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, ukiongozwa na mapikipiki ya ukiwasili katika viwanja vya ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari ya Bumbwini Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja kuhudhuria hafla ya Baraza la Eid  Alhajj lililofanyika Kitaifa Wilaya hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika viwanja vya ukumbi wac Mitihani Skuli ya Sekondari Bumbwini akielekea katika eneo liliandaliwa kupokea Salamu za heshima kutoka katika Gwaride Maalum la Kikosi cha FFU.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein akipokea Salamu ya heshima kutoka katika Gwaride Maalum la Kikosi cha FFU, iliofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
WAZIRI wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, kulihutubia Baraza la Eid Alhajj lililofanyika katika ukumbi wa Mitihani Skuli ya Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika Baraza la Eid Alhajj lililofanyika Kitaifa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja katika ukumbi wa Mitihani Skuli ya Bumbwini.
VIONGOZI wa Serikali na Wananchi wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) akilihutubia katika ukumbi wa mitiha wa Skuli ya Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja lililofanyika Kitaifa mwaka huu.
WANANCHI na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia katika Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
WANANCHI na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia katika Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
WANANCHI na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia katika Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
WANANCHI na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia katika Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
WANANCHI na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia katika Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
WANANCHI na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid Alhajj, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia katika Ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hutuba ya Baraza la Eid Alhajj lililofanyika katika ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiitikia dua
WAUMINI wa Dini ya Kiislam na wageni waalikwa wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya Baraza la Eid Alhajj lililofanyika katika ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein. akiwapungia mkono Wananchi wa Bumbwini baada ya kumalizika kwa hafla ya Baraza la Eid Alhajj lililofanyika Kitaifa katika Ukumbi wa Mitihani Skuli ya Sekondari Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume,baada ya kumalizika kwa hafla ya bara la Eid Alhajj lililofanyika Kitaifa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa hafla ya Baraza la Eid Alhajj lililofanyika katika ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Mahonda.
Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgombea Urais Mteule wa Chama Cha Mapinduzi, CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika sherehe hizo zilizotanguliwa na Swala ya Eid iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Misuka, Mahonda.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na kuzungumza na Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye sherehe hizo zilitanguliwa na Swala ya Eid. 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi na wwageni waalikwa kwenye sherehe hizo zilitanguliwa na Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahonda.
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wakishiriki Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahondawa. 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakiwa katika sherehe hizo. 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakiwa katika sherehe hizo. 
Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahonda ikiendelea. Picha kwa hisani ya Mwinyi2020. 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na viongozi mbalimbali na wageni waalikwa katika sherehe hizo. 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na viongozi mbalimbali na wageni waalikwa katika sherehe hizo. Picha zote kwa hisani ya Mwinyi 2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi waendelee kushirikiana ili wahakikishe kwamba uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu unafanyika kwa amani na utulivu.

Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd El Hajj lililofanyika huko katika skuli ya Bumbwini, Wilaya ya Kaskazini “B”, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambalo lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali pamoja na wananchi.

Alhaj Dk. Shein alisema kwa kufanyika kwa uchaguzi kwa amani na utulivu kutaipelekea Serikali ya Awamu ya Nane itakapoingia madarakani iweze kuyashughulikia maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.

Hivyo, aliwataka wananchi wahakikishe kwamba hatokei mtu au kundi lolote litakalojaribu kuharibu amani hapa nchini, kupandikiza chuki, uhasama na fitna miongoni mwa wananchi na ndani ya jamii yao.

Alhaj Dk. Shein aliwasihi viongozi wa vyama vyote vya siasa na wagombea wao wakati ukifika wajinadi kwa wapiga kura kwa kutangaza Ilani, Sera na Mipango ya vyama vyao.

Aliwasisitiza kuwa ni lazima wahubiri amani, umoja na mshikamano kwa maneno na vitendo, wakijuwa kwamba lengo lao ni kujinadi ili wachaguliwe kwa ajili ya kuiletea maendeleo nchi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, Alhaj Dk. Shein aliwaeleza wananchi kwamba ni wajibu wao kuzingatia, kuheshimu na kuzitii sheria na miongozo ya Uchaguzi inayotolewa na Tume zote mbili za Uchaguzi ambazo ni (ZEC na NEC).

Hivi sasa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika katika mwezi wa Oktoba mwaka huu hivyo, tunapaswa tukumbuke kwamba msingi wa mafanikio yote tuliyoyapata katika awamu zote ni juhudi zetu za pamoja katika kufanya kazi, kuilinda amani na utulivu pamoja na kudumisha umoja na mshikamano”,alisema Alhaj Dk. Shein.

Alieleza kuwa hadi sasa nchi iko shwari, harakati za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinaendelea vizuri na kueleza mategemeo yake kwamba hali hiyo itadumu hadi siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Alisisitiza kuwa iwapo wananchi watafanya hivyo watatoa fursa nzuri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ya kuanza utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo kwa wepesi, hamasa zaidi na ari kubwa ili hatimae iweze kupata mafanikio makubwa zaidi.

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alisema kuwa ili kudumisha na kuuendeleza umoja ni lazima wananchi wajiepushe na tabia mbaya kama kudharauliana,kusengenyana, kuhusudiana, kuhasimiana na kushwawishiana katika kufanya hujuma dhini ya wananchi na Serikali na badaya yake wafanye mambo mema.

Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake za dhati kwa wananchi wote wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla kwa mapenzi makubwa waliyomuonesha na kwa kuiunga mkono Serikali katika kuyatekeleza majukumu yake kwa vipindi vyote viwili vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba.

Alhaj Dk. Shein alitoa shukurani hizo kutokana na kuwa shughuli hiyo ya Baraza la Idd el Hajj iliyofanyika leo huko Bumbwini, Mwenyezi Mungu akipenda itakuwa ni ya mwisho kwake kuhudhudhuria na kutoa hotuba akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Sote tunafahamu kwamba baada ya kufanyika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2020 na kupatikana Rais mwengine wa Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ndio itakuwa mwisho wa uongozi wangu sitoongeza hata dakika moja seuze sekunde moja”alisema Alhaj Dk. Shein.

Aidha, Rais Dk. Shein alisema kuwa katika Ibada ya Hijja mafunzo mengi yanapatikana ikiwemo usawa mbele ya sheria na umuhimu wake katika kutekeleza na kufanikisha mambo mbali mbali katika maisha ya mwanaadamu.

Aliongeza kuwa miongoni mwa mafunzo makubwa yanayopatikana katika utekelezaji wa ibada ya Hijja ni utii wa sheria pamoja na kuimarisha umoja na mshikamano katika hali ya amani na utulivu kwani mambo hayo ndio msingi mkubwa wa mafanikio.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alitoa pongezi kwa viongozi na wananchi wa Bumbwini kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” pamoja na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa ujenzi wa ukumbi uliofanyika Baraza hilo la Idd el Hajj.

Pia, aliuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu ushirikiane na uongozi wa Wilaya ya Kaskazini “B” na Mkoa huo wa Kaskazini kwa ajili ya kulikagua eneo linalokusudiwa kujengwa skuli ya Bumbwini Gongoni kwenye kijiji kipya kwa ajili ya kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi katika skuli ya Bumbwini.

Hivyo, alisisitiza kwamba dhamira ya Serikali hivi sasa ni kujenga Skuli za ghorofa ili kuwepo kwa matumizi bora ya ardhi hivyo, ni vyema suala hilo likazingatiwa katika ujenzi wa skuli hio.

Pia, Alhaj Rais Dk. Shein alisema kuwa ikithibitika kwamba eneo la karibu na Skuli ya Pangatupu linafaa kwa kuzingatia mipango miji na vijiji iliyopo na maendeleo ya muda mrefu ya Mkoa huo, basi aliuagiza uongozi wa Mkoa uanze mradi huo japo kwa kujenga jengo moja dogo kama ni kielelezo cha utekelezaji wa dhamira hiyo.

Halikadhalika, alisema kuwa Mkoa wa Kaskazini Unguja hivi sasa unaongoza hapa Zanzibar kwa kuwa na barabara mpya, nzuri na za kisasa hivyo alitoa pongezi kwa wananchi waliokubali bila ya masharti kupitisha miradi ya ujenzi wa barabara katika mikoa yote ya Unguja na Pemba.

Alhaj Dk. Shein pia, alieleza  juu ya mpango wa ujenzi wa barabara ya Makoba hadi Kiongwe pamoja na barabara ya Bumbwini hadi Mahonda na kueleza kuwa hiyo ni ahadi ya Serikali na kwa vyovyote vile zitatekelezwa.

Kwa upande wa daraja la Mperura linalounganisha eneo la Bumbwini Misufini na Pangatupu lililoporomoka alisema kuwa Serikali inaandaa mipango ya kulifanyia matengenezo daraja hilo katika kipindi kifupi kijacho.

Katika hafla hiyo Alhaj Dk. Shein pia, aliwataka wananchi waliohudhuria Baraza hilo kusimama kwa muda wa dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa aliyefariki usiku wa tarehe 23 Julai na kuzikwa nyumbani kwao Lupaso hapo juzi tarehe 29 Julai, 2020.

Mapema Alhaj Dk. Shein alihudhuria sala la Idd el Hajj iliyosaliwa katika uwanja wa mpira Misuka hapo Mahonda na baadae alisalimiana na Masheikh katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo huko Kinduni.

Viongozi mbali mbali walihudhuria katika Baraza hilo akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassam, Balozi Seif Ali Idd Makamo wa Pili wa Rais, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ambaye pia, ni Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),

Wengine ni viongozi wa dini, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri na Manaibu Mawaziri,Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid  Yahya Mzee, Wabunge, Wawakilishi Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa yote ya Zanzibar, Mabalozi na viongozi wengine wa Serikali, viongozi wa vyama vya siasa, wageni waalikwa na wananchi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, ametumia Baraza la Eid, lililofanyika Bumbwini, Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja kuaga rasmi wananchi wa Zanzibar. Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali. Sherehe hizo zilitanguliwa na Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahonda na kuwataka wananchi waendelee kushirikiana ili wahakikishe Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba unafanyika kwa amani na utulivu.

1 comment:

  1. A very good and informative article indeed . It helps me a lot to enhance my knowledge, I really like the way the writer presented his views. I hope to see more informative and useful articles in future.sport face mask face shield mask running neck gaiter umbrella bougerv

    ReplyDelete

Sharing Buttons

Pages