MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI YAPIGWA FAINI NA TCRA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 2, 2020

MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI YAPIGWA FAINI NA TCRA


MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu kwa makampuni ya simu hapa nchini baada ya kubainika kukiuka kanuni za mawasiliano ya kielectroniki na posta.

Katika taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA),Eng. James Kilaba iliyotolewa leo Julai 02,2020 imesema makampuni hayo ni Airtel Tanzania Plc, MIC Tanzania Plc, Smile Communications Tanzania Ltd, Tanzania Telecommunications Cooperation, Viettel Tanzania Plc, Vodacom Tanzania Plc, na Zanzibar Telecoms Plc.

Taarifa hiyo imesema kuwa hatua hiyo imefikiwa na TCRA baada ya kubaini kuwa makampuni tajwa ya Simu yamekiuka Kanuni Na. 4 & 7(3) za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Ulinzi kwa Mlaji), 2018 na Kanuni Na. 12(4) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Ushuru/tozo), 2018 pamoja na kutozingatia maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na TCRA.

Baada ya kubainika kwa ukiukwaji wa Kanuni hizo na kwa mujibu wa Kifungu cha 48 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Sura ya 172 marejeo ya 2017 ya Sheria za Tanzania, makampuni hayo ni Airtel Tanzania Plc, Zanzibar Telecoms Plc, Viettel Tanzania Plc, MIC Tanzania Plc walitakiwa kufika mbele ya TCRA tarehe 11 Juni 2020 

Ilhali Vodacom Tanzania Plc, Tanzania Telecommunications Cooperation na Smile Communications Tanzania Ltd walifika tarehe 12 Juni, 2020, ili kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria na kikanuni kwa ukiukaji huo wa Kanuni.

 Makampuni hayo yalifika mbele ya TCRA kama yalivyoamriwa.
 Baada ya TCRA kuzingatia utetezi uliotolewa na makampuni yote tajwa hapo juu na kujiridhisha kuwa ni bayana yamekiuka Kanuni, na kwa mujibu wa Kifungu cha 48 (2)&(3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Sura ya 172 marejeo ya 2017 ya Sheria za Tanzania.

TCRA imetoa adhabu kwa makampuni hayo kama ifuatavyo: - Kampuni ya  Airtel Tanzania Plc inatakiwa kulipa faini ya  Shilingi 350,000,000/= (Milioni Mia Tatu na Hamsini) ndani ya siku kumi na nne (14), ikiwa ni pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020.

Kampuni ya MIC Tanzania Plc inatakiwa faini ya Shilingi 300,000,000/= (Milioni Mia Tatu), ndani ya siku kumi na nne (14) pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namnawalivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020.

Kampuni ya Smile Communications Tanzania Ltd kulipa faini ya Shilingi 15,000,000/= (Milioni Kumi na Tano) ndani ya siku kumi na nne (14) pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Kulipa faini ya Shilingi 30,000,000/= (Milioni Thelathini) ndani ya siku kumi na nne (14)pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

 Viettel Tanzania Plc Kulipa faini ya Shilingi 130,000,000/= (Milioni Mia Moja Thelathini)ndani ya siku kumi na nne (14) pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020.

Vodacom Tanzania Plc Kulipa faini ya Shilingi 400,000,000/= (Milioni Mia Nne) ndani ya siku kumi na nne (14) ikiwa pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020.

 Zanzibar Telecoms Plc (ZANTEL) Kulipa faini ya Shilingi 25,000,000/= (Milioni Ishirini na Tano) ndani ya siku kumi na nne (14) pamoja na kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020.

Iwapo Makampuni hayo yatashindwa kutekeleza maagizo haya, TCRA itachukua hatua zaidi za kiudhibiti na kisheria pasipo kutoa taarifa zaidi na kwa gharama zao wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages