MWANAHABARI DOTTO KAHINDI ACHUKUA FOMU UBUNGE CCM BUSANDA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, July 14, 2020

MWANAHABARI DOTTO KAHINDI ACHUKUA FOMU UBUNGE CCM BUSANDA

Dotto Kahindi MKENYE, leo amechukua fomu ya kutia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Busanda. Hapo akipokea fomu hiyo kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Geita, Mwinyikheri Baraza.


MWANAHABARI Dotto Kahindi Mkenye maarufu kama 'Mandolin' leo 14 Julai, amechukua fomu ya kutia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Busanda kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.

Dotto Kahindi Mkenye amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya ya Geita, Mwinyikheri Baraza.

Dotto Kahindi MKENYE ni Mwandishi wa Habari na Masimamizi wa Miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimobiashara, Ufugaji na Biashara.

Tasnia ya Habari amefanyakazi kama Mwandishi kwenye magazeti mbalimbali ikiwemo gazeti la Mwananchi la kampuni ya MCL, na amekuwa mtangazaji wa Radio pia. 


Mbali na Uwanahabari, amekuwa Meneja wa Programu kwenye Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania na sasa ni Meneja wa programu wa Taasisi ya Utamaduni na Maendeleo Africa Mashariki (CDEA).

Ni mwanzilishi wa shule ya Muziki ya Action Music Academy na ni mmiliki wa Promo Online Tv ambayo inatoa Habari za Kilimobiashara na Mazingira.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages