RAIS DKT. MAGUFULI ACHANGIA SHILINGI MILIONI TANO KWA SHULE YA MSINGI SOMANGA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 30, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI ACHANGIA SHILINGI MILIONI TANO KWA SHULE YA MSINGI SOMANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na zawadi yake ya Jogoo alilopewa na Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema Mikidadi Ngenje Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo ya Msingi ya Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi huyo apewe Shilingi laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya kuibua kero ya Shule hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Somanga mkoani Lindi mara baada ya kuwahutubia wakati akitokea Masasi mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi kuhusu ubovu wa barabara ya kutokea Lindi-Somanga wakati alipokuwa akitokea Msibani Masasi mkoani Mwara leo tarehe 30 Julai 2020.
Wananchi wa Nangulukulu wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao wakati akitokea Masasi leo.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Nangulukulu-hadi Somanga mkoani Lindi ambapo sehemu ya barabara yake imeharibika vibaya na kuhitaji matengenezo makubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amechangia Shilingi Milioni 5 kwa Shule ya Msingi Somanga baada Mwanafunzi Rehema Mikidadi Ngenje kuelezea matatizo yaliyopo katika shule hiyo.

Rais Magufuli alitoa fedha hizo na kumkabidhi Mwanafunzi huyo na kutaka apewe shilingi laki moja na fedha inayobaki ifanya ukarabati katika shule hiyo.

Rais Magufuli alisimama Somanga na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo akiwa njiani kurejea Dar Es Salaam akitokea mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages