Ole Sendeka Aaga Rasmi Njombe,Akabidhi Ofisi Kwa RC Mpya - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, July 31, 2020

Ole Sendeka Aaga Rasmi Njombe,Akabidhi Ofisi Kwa RC Mpya

Kushoto ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akimkabidhi baadhi ya nyaraka muhimu za ofisi ya mkoa huo mkuu mpya wa mkoa wa Njombe  mhandisi Marwa Mwita Rubirya kulia wakati wa hafla fupi ya kumuaga Ole Sendeka na kumkaribisha RC mpya wa Njombe iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu huria mjini Njombe
Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akikabidhi mfano wa hundi ya Bilioni 5.397 zilizookolewa kwenye vyama vya ushirika, SACOSS na benki ya wananchi Njocoba kwa mkuu mpya wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Mwita Rubirya pamoja na kamati za usalama mkoa wa Njombe kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kwenda kugawa kwa walengwa.
Baadhi ya wajumbe wa waliofika katika hafla fupi ya kumuaga Ole Sendeka wakimsikiliza aliekuwa mkuu wa mkoa huo wakati akiaga
Ole Sendeka akikabidhiwa Biblia na mkuu mpya wa mkoa wa Njombe kulia ikiwa ni zawadi kutoka kwa wananchi wa mkoa wa Njombe itakayoweza kumsaidia mkuu wa mkoa wa Njombe kusoma neno la Mungu litakalomsaidia katika majukumu yake.

Na Amiri Kilagalila, Njombe


Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amewataka wataalam wa ujenzi wa barabara, madaraja na hata majengo kuacha kufanyakazi kwa mazoea kwa kuwa mkuu mpya wa mkoa aliyeletwa ni mtaalamu wa masuala hayo.

Ole Sendeka ametoa wito huo wakati akifanya makabidhiano ya ofisi ya mkoa wa Njombe kwa mkuu mpya wa mkoa huo na kwamba yeye alifanyakazi kwa kuuliza wataalamu kwenye mambo ya kitaalamu kama ya ujenzi lakini sio mkuu wa mkoa wa sasa.

Kwa hiyo mmeletewa Injinia, huyu hamtacheza naye iwe bara bara za TARURA za TANROADS uwe ujenzi wa majengo yeyote huyu hamtamdanganya”Alisema Ole Sendeka

Pamoja na mambo mengine Ole Sendeka amekabidhi hundi ya zaidi ya shilingi Bilioni tano ambazo ni fedha zilizookolewa toka kwa watu wachache waliofuja fedha za iliyokuwa benki ya wananchi Njombe Njocoba na vyama vya ushirika.

Hi ni hundi ya shilingi bilioni 5.397 ya fedha za wananchi ambazo zimerejeshwa baada ya Rais Dkt,John Pombe Magufuli kwamba wakuu wa miko na wakuu wa wilaya kuhakikisha wale wote waliochukuwa fedha za vyama vya ushirika,vyama vya msingi na SACCOSS wanazirudisha,na leo namkabidhi mkuu wa mkoa wa Njombe ili akaweka utaratibu wa kuzigawa fedha hizi” aliongeza Sendeka

Awali katibu tawala mkoa wa Njombe Catalina Revocati amesema kuwa Ole Sendeka enzi za utawala wake alikuwa kiongozi wa mfano kwa kuwa aliweza kuwaongoza watendaji wake wote kwa kuzingatia maelekezo yake anayoyatoa na kuyafanyia kazi kikamilifu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa mkuu mpya wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Mwita Rubirya amesema anatarajia kuona viongozi wa ngazi za wilaya na halmashauri wanakuwa wa kwanza kutatua changamoto za wananchi kabla hazijamfikia yeye kama kiongozi mkuu wa mkoa.

Tuna wajibu mkubwa kuhakikisha tunasaidia wananchi katika kutatua kero zao,mwananchi anaposhindwa kutatuliwa kero zake hakika anasononeka, sasa nitashangaa kuona kuwa kuna kero ambazo zimetokea katika wilaya Fulani mpaka anayelalamika aipeleke kwenye mamlaka za juu” alisema Rubirya

Mhandisi Rubirya aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe mara baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo kwenda katika majukumu mengine ya kisiasa

1 comment:

  1. A very good and informative article indeed . It helps me a lot to enhance my knowledge, I really like the way the writer presented his views. I hope to see more informative and useful articles in future.RZR Side Mirrors can am x3 side mirrors rzr rear view mirror umbrella bougerv

    ReplyDelete

Sharing Buttons

Pages