MISA YASHAURI WAANDISHI WA HABARI WAPEWE MAVAZI MAALUMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, August 23, 2020

MISA YASHAURI WAANDISHI WA HABARI WAPEWE MAVAZI MAALUMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU



Waandishi wa habari wameliomba jeshi la polisi kutambua uwepo wa waandishi maeneo mbalimbali katika kipindi cha uchaguzi wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migogoro baina ya waandishi na askari hao huku wamiliki wa vyombo vya habari wakishauriwa kutoa mavazi maalumu wakati wa uchaguzi mkuu.

Hayo yamebainishwa katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania uliyofanyika Mkoani Morogoro ili kuweka mahusiano mazuri ya ushirikiano wa kikazi baina ya waandishi wa habari na vyombo vya ulinzi na usalama nchini ambapo, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Salome Kitomali ameshauli iwepo kamati maalumu itakayowaleta pamoja ili kuweza kutatua changamoto zitakazojitokeza katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages