Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Aboubakar Kunenge akizungumza na wananchi wa Pugu Stesheni wakati wa ziara yake iliyofanyika Agosti 10,2020 kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Pugu Stesheni ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.
Katika ziara hiyo RC Kunenge amepokea changamoto mbalimbali ikiwemo za elimu, miundombinu, maji, umeme, afya, migogoro mbalimbali na changamoto za kisheria ambapo zipo alizotatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwaelekea watendaji kuhakikisha wanazishughulikia Mara moja.
Kwenye ziara hiyo RC Kunenge aliambatana na watendaji mbalimbali wa Mkoa akiwemo katibu tawala wa Mkoa, wakuu wa idara pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala.
HABARI PICHA
Wananchi wa Pugu Stesheni wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Kunenge (hayupo pichani) wakati wa ziara yake alipowatembelea wananchi hao J.tatu Agosti 10,2020.

RC Kunenge akisaini Kitabu cha Mahudhurio
No comments:
Post a Comment