Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo TIB, Dkt. Maria Mashingo (wapili kushoto) akimkabidhi zawadi ya mfuko wa katani maalumu kwa ajili ya kutunza mazingira Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) wakati alipotembelea Banda la Maonesho la Benki ya Maendeleo TIB siku ya kilele ya Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Uhusiano wa Kitaasisi, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) na Meneja Masoko na Uhusiano wa Kitaasisi wa TIB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza wakati alipotembelea Banda la Maonesho la Benki ya Maendeleo TIB siku ya kilele ya Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu. Wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Dkt. Maria Mashingo (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Uhusiano wa Kitaasisi, Bw. Patrick Mongella (kulia).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Uhusiano wa Kitaasisi, Bw. Patrick Mongella (kulia) wakati alipotembelea Banda la Maonesho la Benki ya Maendeleo TIB siku ya kilele ya Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Dkt. Maria Mashingo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipotembelea Banda la Maonesho la Benki ya Maendeleo TIB siku ya kilele ya Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu. Anayemsikiliza ni Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Uhusiano wa Kitaasisi, Bw. Patrick Mongella (kulia).
Na Mwandishi wetu, Simiyu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango ametembelea katika Banda la Benki ya Maendeleo TIB wakati wa Siku ya Kilele ya Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mhe. Waziri Mpango alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Dkt. Maria Mashingo.
Mhe. Waziri Mpango alielezwa azma ya ushiriki wa benki hiyo na maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki ya Maendeleo TIB.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe. Dkt. Mpango alitoa wito kwa Benki ya Maendeleo TIB kuendelea kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kutatua sekta ya kilimo nchini.
Benki ya Maendeleo ya TIB imeshiriki maonesho ya Nane Nane ili kutoa elimu kwa umma, kutangaza huduma inayozitoa pamoja na kuvutia wateja wapya kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini. Pia, benki inatumia fursa hiyo kutoa ushuhuda wa miradi ya kimikakati iliyokopeshwa kwa wateja wake waliotapakaa nchi nzima.
No comments:
Post a Comment