Na Richard Mrusha, GEITA
MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesema kuwa Rais Dkt John Magufuli amejitoa sadaka kwa ajili ya nchi hii, hivyo watanzania kuelekea uchaguzi mkuu wahakikishe wanampigia kura nyingi.
Mongella ameyasema hayo Mkoani Geita mara baada ya kutembelea maonyesho ya kimataifa ya Madini ya dhahabu ambapo amesema kuwa Rais Dkt Magufuli amejitoa sadaka kwa kulinda rasilimali za nchi ndio manaa leo Geita imekuwa Kama inavyoonekana.
Amesema kuwa ili kuhakikisha Rais Dkt Magufuli anaendelea kuipaisha Tanzania Oktoba 28, mwaka huu wakamchague kwa Mara nyingine kwa ajili ya maendeleo ya nchi .
"Sote tunajua kwamba huko nyuma matajiri walikuwa hawaguswi lakini nyie wenyewe Leo mnaona wanavyochangia maendeleo na hii yote nikutokana na nidhamu ambayo Rais Dkt Magufuli ameiweka." amesema Mongella.
Amesema kuwa Rais Dkt Magufuli ameweza kusimamia na kudhibiti upotevu wa rasilimali nakwamba amewezesha Sasa watanzania kuonja matunda ya rasilimali zao.
Pia amesema kupitia maonyesho ambayo yanaendelea mkoani humo wao Kama Mwanza wamejifunza na watakuwa mabalozi waziri na ipo siku watafanya.

No comments:
Post a Comment