Kampeni zaanza Burkina Faso kuelekea uchaguzi mkuu Nov 22 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, November 6, 2020

Kampeni zaanza Burkina Faso kuelekea uchaguzi mkuu Nov 22


Rais wa Burkina Faso Roch Marc Chrstian Kabore, amezindua kampeni yake ya kugombea mhula mwingine madarakani, akiahidi kuimarisha usalama na amani nchini humo.

Burkina Faso imekuwa ikikumbwa na mashambulizi kutoka kwa makundi ya wapiganaji kwa mda wa miaka mitano sasa.

Akihutubia wafuasi wake zaidi ya 25,000 mjini Bobo – Dioulasso, Kabore ameahidi kwamba ataendelea kupigana na makundi hayo ya wapiganaji hadi amani itakapopatikana nchini humo.

Anagombea mhula wa pili madarakani na amesema lengo lake kubwa ni usalama wa nchi hiyo.

Roch Marc Christian, anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea wengine 12 katika uchaguzi huo wa Novemba 22.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages