SIMBA SC YAPEWA TIMU YA NIGERIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA HATUA YA AWALI, NAMUNGO KUWAVAA AL-RABAT SC YA SUDAN - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, November 10, 2020

SIMBA SC YAPEWA TIMU YA NIGERIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA HATUA YA AWALI, NAMUNGO KUWAVAA AL-RABAT SC YA SUDAN


Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba SC hatimaye wamepangwa na timu ya Plateau United ya nchini Nigeria katika mchezo ya awali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2020-2021.

Simba SC itaanzia ugenini nchini Nigeria kati ya Novemba 27-29, 2020 wakati itacheza mchezo wa marudiano nchini Tanzania kati ya Desemba 4-6, 2020.

Katika Droo ya Michuano hiyo ilifanyika jioni ya leo katika Makao Makuu ya Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) mjini Cairo nchini Misri, Simba SC imepangwa na timu hiyo ambapo imeelezwa mshindi kati ya Simba SC na Plateau atacheza na Costa do Sol ya Msumbiji au Platinum ya Zimbabwe.

Wakati huo wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho, Namungo FC ya mkoani Lindi watacheza na Al-Rabat Sports Club ya Sudan Kusini katika raundi ya awali ya Michuano hiyo.

Raundi hiyo michezo itapigwa kati ya Novemba 27-29, 2020 na mchezo wa marudiano kupigwa Desemba 4-6, 2020.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages