Uganda yapiga marufuku kundi la uangalizi wa Uchaguzi! - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, November 1, 2020

Uganda yapiga marufuku kundi la uangalizi wa Uchaguzi!

Mamlaka nchini Uganda wamepiga marufuku zaidi ya mashirika 60 yaliyobuniwa kuchunguza uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 kwa misingi kwamba sio halali.

Ofisi ya Kitaifa ya Uganda ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali - ambayo inadhibiti shughuli za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali imesema shirika la kitaifa la uangalizi wa uchaguzi halijasajiliwa.

Ofisi hiyo imesema baadhi ya mashirika chini ya muungano huo hayajasajiliwa wala hayana kibali cha kuhudumu nchini humo

Mkuu wa ofisi hiyo, Stephen Okello, amesema kundi hilo linatakiwa kusitisha shughuli zake mara moja ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa umma.

Raia wa Uganda watashiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge mwezi Januari mwaka 2021.

Shirika la kimataifa la Action Aid nchini Uganda, katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake, limesema kundi hilo lilianzishwa mwezi uliopita kukuza uadilifu katika uchaguzi kuongeza imani ya raia na ushiriki.

Serikali ya Uganda imekuwa ikikosoa mashirika yasiokuwa ya kiserikali kwa kufanya kazi kwa maslahi ya nchi za kigeni kurejelea kazi ya serikali na kuhudumia katika mazingira yasiyoeleweka.

Mwaka 2017, polisi walivamia ofisi za mashirika matatu ya aina hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli haramu za kifedha na uasi ili kudhoofisha nchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages