Wananchi waandamana kupinga kuongezeka gharama za maisha - Angola - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, November 13, 2020

Wananchi waandamana kupinga kuongezeka gharama za maisha - Angola


Polisi katika Mji Mkuu wa Angola, Luanda wametumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji ambao wanapinga kuongezeka kwa gharama za maisha na ukosefu wa ajira.

Watu kadhaa wamekamatwa huku wengine wakijeruhiwa katika maandamano hayo ambayo yalipigwa marufuku na Mamlaka.

Angola ni miongoni mwa wasafirishaji wakubwa wa mafuta Barani Afrika lakini idadi kubwa ya wananchi wake ni masikini.

Hali ya wananchi kutoridishwa na Serikali imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni ambapo kumekuwa na maandamano kadhaa kupinga ufisadi, ajira na unyanyasaji wa Polisi. 

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages