BILIONEA LAIZER AKABIDHI SHULE YA MSINGI ALIYOIJENGA KWA SERIKALI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, January 13, 2021

BILIONEA LAIZER AKABIDHI SHULE YA MSINGI ALIYOIJENGA KWA SERIKALI

Bilionea Saniniu Laizer (Kushoto) akiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary (kulia) kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa Shule mpya ya Msingi aliyoijenga Bilionea hiyo.


Muonekano wa Majengo ya Shule ya Msingi Saniniu Laizer iliyojengwa na Bilionea Saniniu Laizer katika Kijiji cha Naepo kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro.
Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Shule hiyo.


Bilionea Saniniu Laizer (kulia) akimkabidhi hati ya Shule hiyo mwakilishi wa mgeni rasmi katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary (Kushoto) mara baada ya kufunguliwa rasmi Januari 13,2021 Wilayani humo (katikati) ni Mbunge Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendendeka.
Bilionea Laizer akizungumza mbele ya wageni mbalimbali waalikwa na Wananchi wa Wilaya ya Simanjiro Katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Shule ya Msingi Saniniu Laizer, Zuwena Omary akizungumza na hadhara iliyohudhuria kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendendeka akizungumza na Wananchi waliofurika kushuhudia uzinduzi rasmi wa Shule ya Msingi ya Saniniu Laizer uliofanyika Januari 13,2021 Wilayani Simanjiro.



Wananchi mbalimbali wa jamii ya Kimasai kutoka katika kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro na maeneo ya jirani waliohudhuria kwenye hafla hiyo.
Msafara wa Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Bilionea Laizer kwenda kuona nyumba za walimu.
Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary (kushoto) akiteta jambo na Mwenyeji wake Saniniu Laizer.



Muonekano wa Nyumba za Walimu watakaokua wakifundisha kwenye Shule hiyo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO, MANYARA).

Na Richard Mrusha | MANYARA | BILIONEA mtanzania kutoka wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara Saniniu Laizer leo amekabidhi Shule ya Msingi yenye vyumba Saba, Nyumba za walimu nne pamoja na matundu ya vyoo kumi kwa uongozi wa Serikali ya Wilaya hiyo chini ya Mkuu wake wa Wilaya Zephania Chaula .

Shule hiyo ambayo imepewa jina lake la Saniniu imejengwa katika Kijiji cha Naepo kilichopo kata ya Naisinyai Wilayani humo imetumia zaidi ya shilingi milioni 466.8 hadi kukamilika kwake.

Akizungumza wakati akikabidhi Shule hiyo Januari 13,2020 Wilayani humo Bilionea Laizer alianza kwa kuishukuru Familia yake kwa ushirikiano ambao wanaendelea kumpatia huku akiishukuru Serikali kupitia wizara ya elimu katika kumuunga mkono na kumkubalia kujenga shule hiyo na kuipa jina lake.

Laizer amesema kazi hiyo haikuwa nyepesi kwani ni kazi ambayo inahitaji uzalendo ,upendo thabiti dhidi ya Taifa lake lakini kubwa zaidi kujitoa hivyo anashukuru kwa kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ambayo kimsingi aliaza kuijenga mwaka 2017.

"Ndugu zangu leo najisikia fahari kubwa kukabidhi shule hii ambayo kwa asilimia 95 imekamilika na palipobakia ni sehemu ndogo ambapo naamini kwa kushirikiana na serikali tutakamilisha" amesema Laizer 

Nakuongeza kuwa "amejenga vyumba sita vya madarasa kwa shilingi milioni 158, matundu ya vyoo 10 kwa shilingi milioni 26 nyumba za walimu nne kwa maana 4in 2zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa thamani ya shilingi 187 lakini pia vyoo, jiko, ukuta kwenye nyumba za walimu kwa thamani ya shilingi milioni 46 namshukuru sana Mungu." amesema Laizer

Pia ameongeza kuwa atahakikisha eneo lililobakia ambalo ni la ujenzi wa Bwalo, Jiko, uzio na stoo vinakamilika na hiyo nikutokana na ushirikiano uliopo kati ya Serikali na yeye kama mchimbaji wa madini ambaye ameamua kurudisha sehemu ya faida kupitia kile anachokipata.

Katika hatua nyingine Bilionea Laizer ameipongeza wizara ya madini kwa ushirikiano mkubwa wanaompatia hali ambayo imewezesha kufikia hatua aliyonayo na kwamba ataendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi zake kadri atakavyokuwa anabarikiwa .

Amesema ujenzi wa Shule hiyo umegharimu gharama kubwa kutokana na udongo wa eneo hilo lakini pia kiwango chenye ubora wa hali ya juu ambacho kinakidhi matakwa ya shule husika.

"Nimemaliiza kwa kusema ndugu mgeni rasmi kazi hii haikuwa nyepesi nikazi ambayo inahitaji moyo thabiti hususani katika kushirikiana na Jamii inayonizunguka na ahadi yangu nitaendelea kujitoa kadri Mungu atakavyojalia." amesema Laizer.

Kwaupande wake mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ni Karibu Tawala Zuwena Omary kwaniaba ya Serikali amemshukuru Laizer kwa kujitoa kwake na kumwahakikishia kuwa wao Kama Serikali wataendelea kumpa ushirikiano.

Amesema kuwa alichofanya Bilionea huyo ni kitu cha mfano na uzalendo mkubwa na kuna haja ya Watanzania wengine kuendelea kushirikiana na Serikali nakwamba atafikisha shukrani zake kwa Serikali.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages