SHULE ZAFUNGULIWA TENA KENYA BAADA YA MIEZI 9 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, January 5, 2021

SHULE ZAFUNGULIWA TENA KENYA BAADA YA MIEZI 9


Baada ya miezi 9 ya kimya cha kutisha kwenye shule zote nchini Kenya hatimaye Wanafunzi wameanza Muhula wa Pili wa Masomo utakao kamilika katikati ya mwezi Machi mwaka huu. 

Kwa wanafunzi wa shule za chekechea swala la kuvalia Barakoa likawa jambo geni huku Baadhi ya shule zimeripoti changamoto kubwa kutekeleza masharti ya serikali ya kufanikisha masomo wakati wanatekeleza masharti ya maafisa wa afya kudhibithi maambukizi ya virusi vya Corona. 

Hata hivyo kwa wazazi wengi walioathirika kwa janga hilo la Corona nchini humo kibarua cha kuwalipia Karo watoto wao kimekuwa kigumu zaidi. 

Mazingira haya mapya kwa Wanafunzi kuvaa barakoa na kunawa mikono katika hali ya kutii maagizo ya wizara ya afya yanaongeza hofu kwa wanafunzi hao. 

Baadhi ya wanafunzi walipata kujifunza kupitia mtandao walipokuwa nyumbani Waziri wa elimu Profesa George Magoha anatumahi wanafunzi watafidiwa muda wao waliopoteza walipokuwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages