
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekifungia Kituo cha Televisheni cha Wasafi TV kwa miezi sita kwa kukiuka kanuni za maudhui.
Taarifa ya TCRA inasema kituo hicho kilivunja kanuni hizo kupitia kipindi cha TUMEWASHA LIVE CONCERT ambacho kilimuonesha msanii Gift Stanford Joshua a.k.a Gigy Money akinengua kwa mitindo iliyoonesha utupu wa mwili wake.
Aidha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment