MABWENI YA WASICHANA MBONDOLE YAPEWA JINA LA OMARY KUMBILAMO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, January 16, 2021

MABWENI YA WASICHANA MBONDOLE YAPEWA JINA LA OMARY KUMBILAMO

 

Na Mwandishi wetu | DAR ES SALAAM | Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amefanya ziara yake ya kikazi katika Shule ya Secondary Mbondole ambayo imepandishwa hadhi kuwa Shule ya Wilaya.

Katika ziara hiyo Mhe. Meya aliambatana na Afisa Elimu Secondary Manispaa ya Ilala Mwal. Mussa Ally, Diwani wa Kata ya Msongola Mhe. Mwalile pamoja na Diwani wa Viti Maalum Mhe. Magdalena.


Akiwasilisha taarifa yake Mkuu wa Shule ya Secondari Mbondolea alieleza kuwa Mabweni ya wasichana yanahitaji Kujengewa ukuta ili kuongeza ulinzi katika Mabweni hayo, na kununuliwa 'fire Extinguisher', Jokofu la kupozea maji ya kunywa kwaajili ya Walimu pamoja na Tv kwaajili ya wanafunzi wa Bweni, pamoja na kumaliziwa kwa Jengo la Utawala.


Aidha Mwalimu Mkuu huyo alimalizia kusoma taarifa yake kwa kumuomba Mstahiki Meya Kumbilamoto kukubali Mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 yapewe jina lake ambapo Meya Kumbilamoto alikubali.

Akiongea katika hafla hiyo Mhe. Kumbilamoto licha ya kukubali Mabweni hayo kuitwa Jina lake alizipokea Changamoto zote zilizowasilishwa na Mkuu wa Shule hiyo nakuwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo kwani Taifa linawategemea.

"Serikali inafanya mambo mengi katika kuboresha Sekta ya Elimu kwaajili yenu hivyo ni vyema kuzingatia Elimu kwani Taifa linawategemea sana" Alisema Kumbilamoto.

Chanzo, Pugu Online.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages