
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti cha Shukrani Afisa Maendeleo Kata ya Buguruni (Kushoto) kutoka Manispaa ya Ilala kwa kutambua kazi zake alizofanya kwa weledi kwenye kata yake. (wa kwanza Kulia ) ni Mbunge wa Segerea Bonah Kamoli (Picha na Heri Shaaban)
Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akiongea na Mbunge wa Jimbo LA Segerea Bonah Ladslaus Kamoli wakati wa Tathimini ya mikopo Jimbo segerea (kulia)Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri (PICHA na HERI SHAABAN).

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija akipanda bodaboda za mikopo katika maonyesho ya Tathimini ya mikopo Jimbo LA segerea yakioandaliwa na Manispaa ya Ilala January 13/2021 (PICHA NA HERI SHAABAN)
Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiangalia bidhaa za wajasiriamali wakati wa Tathimini ya mikopo Jimbo LA Segerea (kutoka kulia )Afisa Maendeleo Ilala Fransica Makoye na Mkurugenzi wa Manispaa Jumanne Shauri (PICHA na HERI SHAABAN)
Na: Heri Shaaban | DAR ES SALAAM | HALMASHAURI ya Manispaa Ilala mkoani Mkoa wa Dar es salaam inatarajia kufungua Kiwanda cha nyama kitakachoongozwa na Wanawake wa Ilala.
Mikakati ya kufungua kiwanda hicho yamekamilika kitafunguliwa hivi karibuni ofisi zake zitakuwa Vingunguti Jimbo la Segerea .
Akizungumza katika tathimini ya utoaji mikopo ya asilimia kumi ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema amefarijika na Vikundi vya Wanawake waliochukua mikopo ya Serikali wamekuwa waminifu katika urejeshaji hivyo wanawamini kusimamia kiwanda hicho cha nyama.
"Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu za John Magufuli TANZANIA ya uchumi wa viwanda wilaya Ilala iwe na viwanda vya kutosha wanawake wetu wajikwamue kiuchumi " amesema Shauri
Mkurugenzi Shauri alisema mwaka huu katika Jimbo la Segerea wanatoa Bilioni 4, amewataka wasiorejesha warejeshe kwa wakati kabla kuchukuliwa hatua za kisheria hasa makundi ya vijana wengi wasumbufu ndio maana kiwanda tunawakabidhi wanawake.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa Manispaa ya Ilala Fransica Makoye alisema dhumuni la kufanya tathimini ya mikopo kuongeza hamasa kwa vikundi vya mikopo wajue nini kinafanyika jimbo la Segerea maonyesho hayo ya tathimini watafanya kwa mwaka mara mbili
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Ilala Arch, Ng'wilabuzu Ludigija alisema mikopo hiyo mizuri haina riba na kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Ilala na Afisa Maendeleo wa Manispaa ya hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya .
Aliongeza kuwa anaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli hivyo kila mtu aweze kujishughulisha kwa kufanya kazi ili kujipatia kipato cha halali .
Aidha Ludigija alipata fursa ya kutoa tuzo kwa vikundi vilivyorejesha kwa wakati, vya Kata ya Liwiti, Kinyerezi ikiwemo vikundi 30 walioewa vyeti vya kuvitambua.
"Nawataka mtumie fursa hii vizuri ya mikopo ya Manispaa ya Ilala na kurejesha kwa wakati pesa ya serikali kwani lazima irejeshwe ili nawengine waweze kunufaika" Alisisitiza Ludigija.
Nae Mbunge wa jimbo la Segerea Bonnah Kamori alishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Pombe Magufuli kwa kuviwezesha vikundi vya ujasiriamali vya wanawake, vijana na wenye ulemavu jimboni kwake.
Bonnah alitoa Salaam hizo za Shukrani mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu katika maonesho ya shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na wajasiriamali .
"kwa kiasi kikubwa wajasiriamali wa jimbo la Segerea wamenufaishwa na uwezeshwaji unaofanywa na Serikali Kupitia mapato ya ndani ya Hakumshauri yetu" Alisema Bonah.


No comments:
Post a Comment