Mahakama Uingereza yazuia muasisi wa Wikileaks kupelekwa Marekani - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, January 4, 2021

Mahakama Uingereza yazuia muasisi wa Wikileaks kupelekwa Marekani


Mahakama ya Uingereza imekataa ombi la Marekani la kumuhamisha mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange hadi Marekani anapokabiliwa na mashtaka ya ujasusi 

Mahakama ya Uingereza imekataa ombi la Marekani la kumuhamisha mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange hadi Marekani anapokabiliwa na mashtaka ya ujasusi. 

Mahakama imeamua kuwa hatua ya kumuhamisha Assange, ni "ukandamizaji" kutokana na afya yake ya kiakili. 

Jaji Vanessa Baraitser amesema Assange huenda akajiua iwapo atahamishwa hadi Marekani. 

Hata hivyo, serikali ya Marekani imesema itakata rufaa juu ya uamuzi huo. 

Waendesha mashtaka wa Marekani wanamshtumu Assange kwa makosa 17 ya ujasusi na matumizi mabaya ya Kompyuta kwa kuchapisha mtandaoni nyaraka za siri juu ya oparesheni za jeshi la Marekani nchini Iraq na Afghanistan muongo uliopita. 

Iwapo atapatikana na hatia, Assange huenda akapewa kifungo cha miaka 175 jela. 

Julian Paul Assange alizaliwa 3 Julai 1971 ni raia wa Australia ambaye ni mtaalam wa programu za kompyuta na mhariri wa Wikileaks. Hivi sasa anashikiliwa na polisi wa Uingereza kwa kukiukwa masharti ya dhamana aliyopewa 2010. 

Assange alizindua Wikileaks mwaka 2006 na ilipata kufahamika zaidi kimataifa mwaka 2010 baada ya kuvujisha mlolongo wa kashfa zikiwemo za vita vya Afghanistan na vita vya Iraq. Na kufuatia kashfa hizo serikali ya Marekani ilianzisha uchunguzi wa makossa ya jinai dhidi ya WikiLeaks na kuomba msada kwa mataifa washirika. 

Novemba 2010 serikali ya Sweden ilitoa kibali cha kimataifa cha kumkamata Assange ambaye miezi mitatu kabla ya hapo alihojiwa kwa madai ya ukatili wa kingono na ubakaji, madai ambayo Assange aliyakana na kusema atasafirishwa kwenda Marekani kwa sababu ya ushiriki wake katika kuchapisha nyaraka za siri za Marekani. 

7 Disemba 2010 Assange alijisalimisha kwa polisi wa Uingereza lakini aliachiwa kwa dhamana baada ya siku 10 na kwa sababu ya kutofanikiwa harakati za kupinga kusafirishwa kwenda Marekani, alikiuka masharti ya dhamana na kuamua kukimbia . Assange alipewa hifadhi na Ecuador mwezi Agosti 2012 na akasalia kwenye ubalozi wa Ecuador Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages