Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Donald Trump amenaswa kwenye mazungumzo ya simu akimshinikiza Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya jimbo la Georgia amtafutie kura za ziada zaidi ya elfu 12 ili kumsaidia kushinda katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa Urais wa Novemba mwaka uliopita.
Mazungumzo kati yake na kamishna wa uchaguzi Brad Raffensperger ambayo yamechapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza na gazeti la Washington Post, ni hatua ya hivi karibuni inayoonyesha juhudi za Trump kujaribu kumshinikiza afisa wa serikali abadili matokeo ya uchaguzi ili asalie madarakani.
Trump ambaye amekataa kukubali kushindwa na Rais mteule Joe Biden, mara kwa mara alisikika akimsisitiza Raffensperge kubadilisha matokeo yaliyothibitishwa.
Raffensperge alisema Jimbo la Georgia lilihesabu kura zake mara tatu kabla yakuthibitisha ushindi wa Biden kwa kura 11,779.

No comments:
Post a Comment