Chama cha Kihafidhina cha Christian Democratic Union CDU cha Kansela Angela Merkel kimepoteza kura ya kihistoria katika majimbo mawili muhimu nchini Ujerumani.
Matokeo ya uchaguzi huo wa majimbo uliofanyika jana Jumapili huenda yakaamua mustakabali wa siasa za Ujerumani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba.
Kulingana na matokeo ya awali baada ya kura zote kuhesabiwa, katika jimbo la Baden Wüttemberg lililoko kusini magharibi mwa Ujerumani, chama hicho kimepata asilimia 24.1 ya kura huku kikipata asilimia 27.7 ya kura katika jimbo la Rhiland Pfalz.
Katibu Mkuu wa CDU Paul Ziemiak hakuridhishwa kabisa na matokeo hayo.
Ziemiak amesema matokeo hayo yanaonyesha pingamizi na ukosefu wa subra kuhusiana na jinsi janga la virusi vya corona linavyoshughulikiwa Ujerumani.

No comments:
Post a Comment