SYRIA YAADHIMISHA MIAKA KUMI TANGU MAANDAMANO YA KUMPINGA ASSAD - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, March 15, 2021

SYRIA YAADHIMISHA MIAKA KUMI TANGU MAANDAMANO YA KUMPINGA ASSAD


Nao Raia wa Syria leo wanaadhimisha miaka kumi tangu maandamano ya amani dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad Machi 2011 kuzuka na kugeuka kwa haraka na kuwa vuguvugu lililopelekea kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Licha ya mwongo mmoja wa mapigano na nchi iliyosambaratika, Assad bado amekwama madarakani. Uchumi wa Syria kwa sasa umedorora kabisa na nchi hiyo imegawanyiika katika sehemu tatu.

Kundi moja lililo na mafungamano na al-Qaeda linadhibiti mkoa wa Idliba kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, huku waasi wanaoungwa mkono na Uturuki wakiwa wanadhibiti sehemu kadhaa katika mpaka wa Syria na uturuki.

Majeshi ya Kikurdi yanayoungwa mkono na Marekani yanashikilia karibu robo ya nchi kaskazini mashariki na sehemu iliyosalia inadhibitiwa na Assad.

Vita hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu nusu milioni huku nusu ya idadi jumla ya Wasyria kabla mapigano hayo iliyokuwa milioni 23, wakiwa wameachwa bila makao.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages