
- Ni baada ya mwitikio wa wananchi kutaka Chanjo kuwa mkubwa.
- Asema wahusika ni Wananchi wote Wenye Umri wa kuanzia miaka 18 kuendelea.
- Awahakikishia wote watakaofika watapata Chanjo na cheti kinachotambulika kimataifa.
- Awaelekeza Wakuu wa Wilaya nao kutenga siku Maalumu ya utoaji chanjo.
Kufuatia mwitikio mkubwa wa Wananchi kuhitaji huduma ya kupata Chanjo ya Corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesikia kilio hicho na kuamua kutenga siku ya Jumapil ya Agost 22 kuwa siku Maalumu ya zoezi la wazi la utoaji wa Chanjo ya Corona kwa Mkoa huo kwenye Uwanja wa Uhuru ili kuwezesha wananchi waliokuwa wakikosa nafasi Kutokana na foleni au majukumu ya kazi Waweze kupata huduma hiyo.

RC Makalla amesema zoezi Hilo litaanza kuanzia saa mbili Asubuhi Hadi saa kumi jioni na litahusisisha wananchi wa Umri wa kuanzia miaka 18 kuendelea na endapo foleni itakuwepo watatoa huduma Hadi apo watakapohakikisha watu wote waliojitokeza wamehudumiwa.
Aidha RC Makalla amesema zaidi ya Watoa huduma 100 watasimamia zoezi Hilo na vyeti vitatolewa hapohapo uwanjani.

Hata hivyo RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya nao kuandaa siku Maalumu ya utoaji wa Chanjo kwenye eneo Maalumu ndani ya Wilaya zao ili kuwafikia wote wanaohitaji Chanjo.
No comments:
Post a Comment